Na Esther Macha, Mbarali
WATU wawili wamefariki dunia katika matukio tafauti Mkoani Mbeya likiwemo la wakala wa pembejeo za kilimo katika kata ya ubaruku kuuwa kwa kupigwa risasi na majambazi nyumbani kwake na mwingine kuuwa na wananchi baada ya kuiba ng,ombe tisa.
Akizungumza na gazeti jana , Kaimu kamanda wa polisi Mbeya Mrakibu msaidizi wa polisi Bw. Anacletus Malindisa alisema kuwa tukio la kwanza lilitokea majita saa7.40 usiku katika kijiji cha Mkunywa katika kata ya Madibira majambazi walivamia nyumbani kwa mfanyabiashara wa duka na kumpiga kwa risasi.
Kaimu kamanda huyo alimtaja marehemu aliyeuwawa kuwa ni Ruben Msigala (42) ambaye alipigwa risasi mbili tumboni na kupoteza maisha papo hapo.
“Hawa wauaji haijajulikana mapema kama kuna vitu vyovyote ambavyo wamechukua lakini jeshi la polisi bado linafanya uchunguzi kujua kama majambazi hayo yamechukua kitu chochote kwenye nyumba ya mfanyabiashara huyo”alisema Kamanda huyo.
Aidha Bw. Malindisa alisema majambazi hayo baada ya kufanya mauaji hayo ya kutisha walimjeruhi kwa kipigo mke wa marehemu Bi.Edelin Msungu ambaye amelazwa katika hospitali ya madibira.
Alisema mama huyo bado anaendelea na matibabu katika hospitali kwa majereha aliyopata baada ya kupata kipigo kutoka kwa wauaji hao.
Hata hivyo aliongeza katika tukio lingine mtuhumiwa wa wizi wa mifugo aitwaye Moku Malungo (41) mkazi wa Ibumila Rujewa aliuwawa kwa kupigwa na wananchi wenye hasira kali baada ya kubainika kuiba ng,ombe.
Alisema mtuhumiwa huyo alipata kipigo hicho baada kuwacharanga kwa sime wananchi waliokuwa wakimfuatilia nyendo zake baada ya vkuiba ng,ombe 9 kutoka wilayani chunya.
No comments:
Post a Comment