Bi. Sophia Urio |
Msanii mahiri wa ngoma za asili Tanzania, Salum Wanne ‘Wanne Star’, amedai kuwa ametapeliwa fedha zake na Bi. Sophia Urio ambaye ni muandaaji wa Shindano la Vodacom Miss Arusha City Center 2011 yaliyofanyika Mei 13, 2011 katika ukumbi wa Triple A, Arusha.
Akizungumza leo, Wanne Star alisema kuwa anasikitika sana kutapeliwa na muandaaji wa shindano hilo, kwa kitendo cha kumkimbia mjini Arusha pindi alipoenda kufanya onyesho kwenye shindano hilo ambalo yeye (Bi Sophia Urio) alikuwa ni muandaaji wa shindano hilo.
Akisimulia mkasa huo, msanii huyo alibainisha kuwa "Kiukweli sikutarajia kama Mwanadada yule angeweza kunitapeli, kwani tulifika mjini Arusha na akatupokea vizuri na kutupeleka hoteli kwa ajili ya maradhi,tukalala na siku iliyofuata tukaenda kufanya kazi kwenye shindano lake, tulipomuuliza kuhusu malipo alidai kuwa angetupa wakati wa shoo itakapoisha,lakini cha ajabu baada ya shoo kuisha hakuonekana,hali ambayo ilitupelekea kuwa na wasi wasi,tulipokuwa tukijaribu kumpigia simu hakupokea na baadae akazima, kesho yake simu yake haikupatikana kabisa hali iliyopelekea sisi kuanza kuhangaika huku na kule tukimsaka,"
Wanne Star anasema baada ya kubaini hali imekuwa teteu kwa upande wao,wakamfuata Dj Charles Muhamiji (Meneja wa Clouds FM tawi la Arusha) na kuwapatia msaada wa nauli na hatimaye kufanikiwa kurudi jijini Dar es Salaam lakini kwa mbiinde.
Alipoulizwa ni juhudi gani alizifanya kwa minajili ya kuipata hela yake, msanii huyo alianza kusononeka huku akionyesha sura ya huzuni na kusema kuwa yote anamwachia Mungu kwa vile jasho la mtu huwa halipotei bure. 'Mpaka sasa nikijaribu kumpigia simu simpati,sasa sijui amebadili namba yake ya simu ama la.! lakini kimsingi hakufanya utu kabisa,lakini ndiyo kama nilivyosema kwamba jasho la mtu huwa halipotei bure,ipo siku tu'alibainisha Wanne Star.

Katika mahojiano yaliyofanywa na blog hii na baadhi ya washiriki wa shindano hilo wamelalamika kutolipwa pesa zao jambo ambalo walikiri wazi kuwa halikuwa la kiugwana kabisa,aidha mmoja wa washiriki (jina kapuni) alisema kuwa mpaka sasa hawajalipwa kitu na hawajui mustakabali wa malipo yao. "Tumechoka.! mpaka sasa hatujalipwa na hatujui itakuwaje kuhusu malipo yetu, ndiyo maana tumeleta kilio chetu kwenye vyombo vya habari ili wahusika wakuu wajue na watusaidia katika hilo," alisema mshiriki huyo.
Kama vile haitoshi, pia kuna kijana mmoja (jina kapuni) alisema kuwa hata yeye amefuatilia malipo yake, kila akipiga simu majibu yake huwa nitakulipa... nitakulipa, mara aambiwe hela yote amelipa deni Naura Springs hoteli ,jambo ambalo halikuwepo kwenye makubaliano yao ya kazi na limekuwa likimkera sana. Mpaka sasa ni takribani ni miezi mitatu tangu shindano hilo lifanyike jijini Arusha,na baadhi ya watu wengine wamekuwa wakilalamikia kutolipwa kwa namna moja ama nyingine,hali ambayo imeonyesha dhahiri ni kutapeliwa.
Habari kwa hisani ya Habari na matukio Blog

No comments:
Post a Comment