WAFANYABIASHARA SOKO LA MBALIZI WATISHIA KUTOLIPA KODI
Na Joachim Nyambo,Mbeya.
WAFANYABIASHARA katika soko A la Mbalizi wilayani Mbeya wametishiakuacha kutoa malipo ya aina yoyote ikiwemo kodi kwa halmashauri yaoiwapo halmashauri hiyo itaendele kufumbia macho tatizo la ukosefu wachoo bora katika soko lao.Kauli hiyo ya wafanyabiashara na wateja katika soko hilo inakujakufuatia hali ya hatari inayozikabili afya zao kufuatia choo kilichopokufurika uchafu kiasi cha maji taka kutoka kwenye choo hichokutiririka katika vyumba na vibanda vyao.RFA imetembelea sokoni hapo leo na kujionea hali halisi ambapo choohicho kinaonekana kutonyonywa uchafu kwa muda mrefu na maji machafuyakitiririka huku vyumba vya kutolea huduma za vyakula hususanimigahawa na Bucha vikiwa jirani na pia ukuta wa choo hicho ukiwa naufa mkubwa unaoweza kusababisha kubomoka wakati wowote.John Mjafa ni mmoja wa wafanyabiashara wahanga wa hali hiyo ambayebaada ya kufungua chumba chake cha stoo Rfa ilijionea maji machafukutoka katika choo hicho yakiwa yamezagaa kwenye chumba hicho nakumiminika hadi nje kuliko na kibanda alichopanga bidhaa zake zaviatu.Akizungumzia hali hiyo,Mjafa amesema kila siku amekuwa akilazimikakumwaga mchanga mkavu ili unyonye maji hayo na baadaye kuuzoa huku piaakilalamikia harufu mbaya ya majitaka hayo kuwa imekuwa kero kwake nawafanyabiashara wengine.Naye mmoja wa wauzaji wa chakula katika eneo hilo mwenye mgahawa waMakenza,Neema Jackson amesema hali hiyo inaweza kuwa chanzo chamagonjwa ya mlipuko hususani kipindupindu.Kwa upande wake mwenyekiti wa soko hilo Grace Nyato amesema ni mudamrefu umepita tangu choo hicho kinyonywe uchafu na walikwisha toataarifa kwa mkurugenzi wa halmashauri Juliana Malange aliyeahidikulishughulikia.Mkurugenzi Juliana Malange hakupatikana ofisini kwake na hataalipopigiwa simu yake ya kiganjani hakuwa tayari kupokea.
No comments:
Post a Comment