Harakati za awali kuelekea kupata wagombea wa udiwani katika uchaguzi mdogo katika Kata ya Majengo na Nzovwe jijini Mbeya kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) zinaendelea vizuri baada ya chama hicho kukamilisha uchaguzi wa awali wa wagombea.
Akizungumza na mwandishi wetu Katibu wa CCM Wilaya ya Mbeya Mjini Bi.Bahati Makalanzi amesema kura za maoni za Kata zimeshafanyika na kwamba wagombea wote watajadiliwa ili kupitishwa katika vikao vya halmashauri ya mkoa.
Ameongeza kuwa kata ya Majengo ilikuwa na wagombea 6 ambao walikuwa wakiwania nafasi ya kukiwakilisha chama Cha Mapinduzi katika uchaguzi mdogo ambapo SAMUEL MWAMBONA alipata kura 188 DAUSEN MSHILU kura 48 HASSAN MWALUKINDI kura 28 JOSEPPH MWAMBAPA kura 28 FILIMON MWAISOLEKA kura 12 na RAISON MWASEMBO kura 7.
Kwa upande wa kata ya Nzovwe wagombea walikuwa watano ambapo ISAAC SINTUFYA alipata kura 127 GENNER MWAIJANDE kura 96 LUCIUS LUOGA kura 60 FRED MWAKATENYA kura 41 na KELLY SICHONE kura 3.
Kampeni za uchaguzi mdogo kwa ajili ya kuziba nafasi ya madiwani wa kata hizo zitafanyika kwa muda wa siku 21 ambapo zitaanza septemba kumi na uchaguzi kufanyika octoba pili mwaka huu.
No comments:
Post a Comment