Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, August 19, 2011

TIMU YA UMISSETA NYANDA ZA JUU YATAMBA KUFANYA VEMA MASHINDANO YA AFRIKA MASHARIKI NA KATI

Na Joachim Nyambo,Mbeya.
TIMU ya soka ya umoja wa shule za sekondari(Umisseta) kanda ya nyanda
za juu kusini iliyofuzu katika mashindano hayo ngazi ya taifa imetamba
itaiwakilisha vizuri Tanzania katika mashindano ya Afrika Mashariki na
kati kwa shule za sekondari.

Mashindano hayo yanatarajia kuanza agost 25 mwaka huu Mbarala nchini
Uganda huku timu hiyo ikitarajia kuanza safari mapema wiki ijayo
kuelekea jijini Mwanza watakakokutana na timu nyingine za kanda ili
kuunda timu ya taifa.

Akizungumza na mwandishi wetu jana (Agost 18) kocha wa timu hiyo Amos
Chiwaya alisema mazoezi wanayoendelea kufanya wachezaji wa timu hiyo
ikiwa ni wiki moja sasa tangu waingie kambini yametosheleza kuwajenga
na kutoa uhakika wa timu kufanya vizuri.

Kocha huyo alisema kikosi chake kina jumla ya wachezaji 21 akiwemo
Michael Mpesa aliyechaguliwa katika timu ya taifa ya timu ya vijana
walio na umri wa chini ya miaka 17 atakayeungana na wenzake jijini
Mwanza baada ya timu kuwasili.

Timu hiyo inaundwa na wachezaji kutoka mikoa miwili inayounga kanda
hii ambapo kutoka Rukwa wapo wachezaji sita wakati Mbeya 15 pamoja na
mmoja atakayekwenda kushiriki mchezo wa riadha katika mita 100.

No comments: