Na Esther Macha, Mbarali
MKUU wa Mkoa wa Mbeya Bw. John Mwakipesile amewataka wakurugenzi wa halmasahauri na wakuu wa wa idara kusimamia sheria na miongozo ya serikali kuhusu ukusanyaji wa mapato na matumizi ya fedha za halmashauri ili fedha zinazotolewa na serkali kwa ajiri ya shughuli za maendeleo ziweze kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa..
Bw.Mwakipesile aliyasema hayo jana wakati wa kikao cha baraza la madiwani cha kujadili taarifa ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali ambacho kilifanyika katika ukumbi wa maji uliopo Wilayani hapa.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa ni vema wakurugenzi na wakuu wa idara wakasimamia zoezi9 hilo la kusimamia sheria hiyo ili fedha za miradi zinazotolewa na serikali kwa ajiri ya kusaidia shughuli za wananchi ziweze kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
“Hali hii ndugu zangu itaziwezesha halmashauri kuendlea kupata fedha za maendeleo na nyingine zinazotolewa kwa kuzingatia sifa nzuri za utunzaji wa fedha za miradi na kufuata sheria na kanuni zilizowekwa na halmashauri zao”alisema Bw. Mwakipesile.
Hata hivyo Bw. Mwakipesile aliongeza kuwa fedha hizo zinapaswa kupelekwa na kutimiza m,alengo yaliyokusudiwa kwa manufaa ya walengwa wakuu ambao ni wananchi .
Alisema kuwa Mkurugenzi na wakuu wa idara ndio wasimamizi wakuu wa fedha za miradi ya maendeleo hivyo kama wakuu wa halmashauri wanatakiwa kutojihusisha na mipango yeyote ile mibaya ya matumizi ya fedha za serikali yasiyozingatiwa sheria na kanuni taratibu .
“”nitoe angalizo kwenu nyinyi viongozi kuungana pamoja kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za serikali ikutekeleza jukumuy la kuwainua wananchi na kuwawezesha kujiletea maendeleo “alisema Bw. Mwakipesile.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya alisema kuwa viongozi na watendaji katika ngazi za chini wanapawa kupatiwa ujuzi na stadi za kazi za utunzaji wa fedha na kutumia vizuri na ni vema halmashauri zikabuni mafunzo mazuri kulingana na na uwezo wa viongozi hao.
Kwa Upande wake Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbarali Bw. George Kagomba alisema halmashauri imekuwa ikifuata kanuni na miomgozo ya serikali ya ukusanyaji wa mapato ya halmashauri.
No comments:
Post a Comment