Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, August 29, 2011

Mbunge wa Mvomero aingilia kati mgogoro wa Ardhi Kipera


Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makala akimsikiliza Bibi Mawazia Kibwana , mkazi wa Kitongoji cha Kinyenze, Kijiji cha Kipera, Tarafa ya Mlali, Wilaya ya Mvomero, akitoa malalamiko kwa Mbunge wake juu ya kitendo cha kubomolewa choo chake na Mwekezaji Raia wa kigeni na kuzungusha uzio uliofikia upenuni mwa makazi yake. Mbunge huyo alitembelea kitongoji hicho mwishoni mwa wiki kujionea hali halisi ya mgogoro wa ardhi uliopo kijijini hapo.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Mkoani Morogoro, Amos Makala (kushoto) akikagua uzio uliowekwa na Kampuni ya Tanbreed Poultry Limited inayomilikiwa na Mzungu aliyenunua shamba Kitogoji cha Kinyenze, Kijiji cha Kipera, Tarafa ya Mlali, Wilaya ya Mvomero na kuzua mgogoro mkubwa wa mipaka baina yake na wananchi wa eneo hilo. Anaemuongoza ni Said Ahmad mkazi wa Kinyenze.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makala akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Kinyenze, Kijiji cha Kipera, Tarafa ya Mlali, Wilaya ya Mvomero, Morogoro mwishoni mwa wiki katika harakati za kutatua mgogoro wa ardhi uliopo kijijini hapo , kufuatia mwekezaji Raia wa kigeni kuuziwa eneo kubwa la ardhi na kumega sehemu ya mashamba yao, kufunga barabara, shule na kubomoa baadhi ya vyoo vya wakazi wa kijiji hicho
Afisa Ardhi wa Wilaya ya Mvomero, Majaliwa Jafari akijibu hoja za wakazi wa Kitongoji cha Kinyenze, Kijiji cha Kipera, Tarafa ya Mlali, Wilaya ya Mvomero, Morogoro mwishoni mwa wiki wanaolalamika juu ya kuvamiwa na mwekezaji Raia wa kigeni kuuziwa eneo kubwa la ardhi na kumega sehemu ya mashamba yao, kufunga barabara, shule na kubomoa baadhi ya vyoo vya wakazi wa kijiji hicho. Kushoto ni Mbunge wa Mvomero, Amos Makala na katikati ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Kipera Anthony Karoli
Wananchi wa Kitongoji cha Kinyenze, Kijiji cha Kipera, Tarafa ya Mlali, Wilayani Mvomero, wakiwa katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makala aliyefika kijijini hapo mwishoni mwa wiki kufuatilia mgogoro wa ardhi ulipo kati ya wananchi hao na mwekezaji raia wa kigeni aliyenunua shamba kijijini hapo na kuweka uzio na kufunga njia na mashamba yao.(Picha na Mroki Mroki).

============== ========== ================
Mbunge wa Mvomero aingilia kati mgogoro wa Ardhi Kipera
*atoa wiki moja maofisa ardhi kumaliza tatizo au waende mahakamani

Na Mroki Mroki, Mvomero
MBUNGE wa jimbo la Mvomero, mkoani Morogoro, Amos Makala ameingilia kati mgogoro wa ardhi uliopo katika Kitongoji cha Kinyenze , Kijiji cha Kipera, Tarafa ya Mlali , Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro baina ya wananchi na mwekezaji wa Kigeni aliyeuziwa shamba kijijini hapo.

Akizungumza mwishoni mwa wiki Kijijini hapo Makala aliyeambatana na Ofisa Ardhi wa Wilaya hiyo, Majaliwa Jaffari amewataka idara ya ardhi kuchukua hatua za haraka na dharula kutatua mgogoro huo kabla ya kuibuka kwa machafuko ya uvunjifu wa amani.

“Nimejionea mwenyewe baada ya kusikia kilio chenu juu ya mwekezaji huyu, watu wa ardhi tafadhalini sana lishughulikieni suala hili haraka sana na mkae pamoja mgogoro huu umalizike upesi iwezekanavyo, ndani ya wiki moja tatizo hili liwe limemalizika”, alisema Makala.Zaidi Bofya Hapa

No comments: