Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Saturday, August 27, 2011

Mbarali Hatarini kupata hati yenye mashaka




Na Esther Macha, Mbarali
 
SERIKALI mkoani Mbeya imesema kuwa halmashauri ya wilaya ya Mbarali imepata hati yenye mashaka kwa mwaka 2009/2010 kutokana na kutotumika kwa miradi  ya wananchi  iliyokamilika yenye thamani ya sh.mil.359,226,370 na fedha kutumika vibaya pasipo kukidhi mahitaji ya huduma iliyokusudiwa.
 
Imeelezwa kuwa kitendo cha kupata hati yenye mashaka kwa halmashauri hiyo kumesasabisha miradi ya maendeleo kushindwa kufanya kazi licha ya kukamilika mapema lakini imekuwa haifanyi kazi kwa uzembe wa watu wachache.
 
Hayo yalisemwa juzi na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya John Mwakipesile wakati wa kikao cha kujadili taarifa ya Mkaguzi na mdhibiti  Mkuu wa hesabu za serikali kilichofanyika katika ukumbi wa maji uliopo wilayani hapa ..
 
“Jambo jili halikubaliki na linaonyesha namna ambavyo watendaji wameshindwa kusimamia vema fedha za maendeleo na kukosekana kwa ubunifu wa usimamizi wa miradi ya maendeleo hali iliyopelekea Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa  hesabu za serikali kubaini mapungufu mengi katika taarifa  ya ukaguzi ya mwaka 2009/2010”alisema Mkuu huyo wa Mkoa.
 
Hata hivyo Bw. Mwakipesile alisema kuwa  miradi mingine ya maendeleo  ambayo ambayo haikukamilika ni  miradi ya kilimo , ujenzi wa nyumba  ya mwalimu,ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari Utengule Usangu .
 
Alisema mambo mengine ambayo yamesababisha halmashauri ya Wiulaya ya Mbarali kupata hati yenye mashaka ni kutofuatwa kwa sheria ya manunuzi ya mwaka 2004 na marekebisho yake ya mwaka 2005 na halmashauri kushindwa kujibu hoja ya mkaguzi kwa wakati.
 
“Wakaguzi wanafika kudai nyaraka Fulani unaambiwa hamba lakini baada ya siku mbili nyaraka hiyo inapatikana ikiwa sehemu nyeupe kabisa sasa  hii tabia si nzuri  ndungu zangu watendaji  nyaraka zote lazima ziwepo kwenye ofisi ya Mhasibu wa halmashauri  ili kuondoa wasi wasi kwa wakaguzi”alisema .
 
Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa kwa mwaka 2009/2010  kati ya halmashauri  saba ni halmashauri mbili ndizo zimepata hati zenye mashaka  ambazo ni Mbarali  na Halmashauri ya Jiji la Mbeya, hivyo makosa hayo hayatakiwi kujirudia tena  katika halmashauri hizo.
 
Aidha Bw. Mwakipesile alizitaka halmashauri hizo kutorudia makosa hayo tena  ya kupata hati yenye mashaka kwa mwaka 2010/2011 na kuwa ni muhimu makosa hayo yakarekebishwa mapema.
 

No comments: