Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, August 8, 2011

Kampuni ya mbegu ya NOSCOL yaonesha mbegu bora za mahindi kwa wakulima

Mkurugenzi wa kampuni ya kuzalisha mbegu ya Northern Seed Co,ltd Arson Shangali akiwaonesha wakulima mashamba mawili ya mahindi yaliyopandwa mbegu tofauti za mahindi.
Wakulima wakiangalia tractor linalotumika kubeba Mahindi mara baada ya kuvunwa shambani siku ya maonesho ya wakulima yaliyofanyika Kimashuku mkoani Kilimanjaro.
Mkurugenzi wa makampuni ya mbegu Tanzania ,Baldwin Shuma akizungumza na wakulima (Hawapo pichani) wakati wa maonesho ya wakulima yaliyofanyika Kimashuku mkoani Kilimanjaro.
Afisa Kilimo na Mifugo kata ya Machame Richard Kessy akitoa ufafanuzi kwa wakulima juu ya mbegu za mahindi zinazo himili uhaba wa mvua kutoka kampuni ya NOSCOL.
Wakulima na wafugaji kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kilimanjaro wakifuatilia maelezo kutoka kwa mmoja wa wazalishaji wa mbegu (hayupo pichani).
Baadhi ya wakulima wakitembelea banda la maonesho ya wakulima kutizama mbegu bora zinazozalishwa na kampuni ya NOSCOL.
Mfanyakazi wa kampuni ya mbegu ya NOSCOL,Reggy Masawe akimuonesha mmoja wa wakulima wa Kimashuku aina bora ya mbegu za mahindi wakati wa maonesho ya wakulima yaliyofanyika Kimashuku mkoaniKilimanjaro.
Wakulima wakiwa katika picha ya pamoja siku ya maonesho.Picha na Dixon Busagaga.
Habari kwa hisani ya Mtaa kwa Mtaa Blog

No comments: