Jeshi la polisi mkoani Mbeya limewataka wafanyabishara mkoani Mbeya kuacha mara moja kutumikisha watoto kwenye shughuli zao kwani kitendo hicho ni kinyume cha sheria.
Msemaji wa Jeshi la polisi mkoa wa Mbeya Inspekta Majaliwa amesema jeshi la polisi halitovumilia kuona mtoto mdogo akifanyishwa kazi badala ya kupelekwa shule.
Baadhi ya watoto waliokutwa wakifanya shughuli mbalimbali zikiwemo za uuzaji wa mitumba na usambazaji wa chakula kinachopikwa na akina mama lishe wamesema kupitia shughuli hizo wamekuwa wakipata fedha kwa ajili ya kununua mavazi, madaftari na chakula.
No comments:
Post a Comment