Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, August 9, 2011

HAFLA YA KUFUTURSHA WANAFUZNI WA MADRASA NA YATIMA MAFIA


Wanafunzi wa Madrasatul Shamsia ya Mjini Mafia wakipokea kwa furaha katoni ya sabuni kutoka kwa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba.Vodacom kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii wa Vodacom Foundation ilitoa pia sadaka ya vyakula kwa ajili ya futari kwa wanafunzi zaidi ya mia tatu wa madrasa mbalimbali wilayani humo pamoja na kuwafuturisha mwishoni mwa wiki.Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule (katikati) na Imam Mkuu wa Msikiti mkuu wa Wilayani Ally Mwabaku.
. Mkuu wa mfuko wa kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom wa kusaidia jamii wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule akimhudumia moja ya waumini wa dini ya Kiislamu wakati wa hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na mfuko huo katika msikiti mkuu wa wilaya Qadiriya na kuhudhuriwa na waislamu mbalimbali wakiwemo watoto zaidi ya mia tatu kutoka madrasa za mjini na vijijini zilzopo wilayani humo ikiwa ni sehemu ya kampeni ya Vodacom share and care ambapo kwa mwezi wa mfungo wa Ramadhani hulenga kufuturisha waislamu sehemu mbalimbali na kutoa sadaka ya futari kwa yatima na wajane.
Meneja Mawasiliano wa kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania Salum Mwalim akimhudumia futari shekhe Mkuu wa Wilaya ya Mafia Sheikh Yusuf Selemani wakati wa hafla ya kufuturisha wasilamu na watoto wa madrasa kisiwani Mafia iliyoandaliwa na Vodacom Foundation ambayo ni sehemu ya kampeni ya Vodacom ya kila mwaka ya share and care ambapo kwa mwezi wa mfungo wa Ramadhani hulenga kufuturisha waislamu sehemu mbalimbali na kutoa sadaka ya futari kwa yatima na wajane.
Wanafunzi wa Al-Madrasatul Hairislamia ya Mjini Mafia kwa furaha wakibeba kiloba cha mchele mara baada ya kukabidhiwa msaada wa sadaka ya futari kwa ajili ya mfungo wa Ramadhani.
.Wanafunzi wa Al-Madrasatul Hairislamia ya Mjini Mafia kwa furaha wakibeba kiloba cha mchele mara baada ya kukabidhiwa msaada wa sadaka ya futari kwa ajili ya mfungo wa Ramadhani. Vodacom kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii wa Vodacom Foundation ilikabidhi sadaka kwa wanafunzi zaidi ya mia tatu wa madrasa mbalimbali za kisiwani Mafia yenye thamani ya zadi ya shilingi milioni tisa ikiwa ni sehemu ya kampeni ya Share and Care ambapo kwa mwezi wa Ramadhan hulenga kufuturisha waislamu na kutoa sadaka ya futari kwa watoto hususan yatima na pia wajane.
Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akikabidhi sehemu ya sadaka ya futari kwa watoto wa madrasa za wilayani Mafia yenye thamani ya zadi ya shilingi milioni tisa. Vodacom kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii wa Vodacom Foundation ilikabidhi sadaka ya futari kwa watoto zaidi ya mia tatu wa kisiwani Mafia hafla iliyoambatana pia na kufuturisha katika msikiti mkuu wa Wilaya mwishoni mwa wiki. Wanaoshudia makabidhiano hayo ni Mkuu wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule na Imam Mkuu wa Msikiti wa Wilaya Ally Mwabaku.


No comments: