Zaidi ya shilingi milioni 17 zimekusanywa na Chama cha Wafanyakazi wa Mawasiliano na Uchukuzi nchini Tanzania [COTWU(T)] Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, katika kipindi cha miaka 2005 hadi 2010 zilizotoka na ulipaji wa ada za wanachama.
Taarifa ya Chama hicho kwa Mgeni rasmi wa Mkutano wa Nne wa COTWU(T) Naibu Katibu Mkuu Taifa, Buhare Semvua aliyekuwepo katika mkutano huo ambao uliambatana na uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti na sekta ndani yake Kanda ya Nyanda za Juu kusini imesema shilingi milioni 17, 944,029 zimekusanywa kutokana na makato ya mishahara.
Mwaka 2005 pekee chama hicho kilikusanya kiasi cha shilingi milioni 14,837,024.70 hadi mwaka 2010 kiasi cha shilingi milioni 17, 944,029.00.
Taarifa hiyo imebainisha kuwa mpaka sasa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ina matawi 15 katika mikoa ya Mbeya, Iringa na Ruvuma, huku wakitarajia kuongeza zaidi mengine ili kuwasaidia wafanyakazi wanaonyanyaswa na waajiri wao.
Kwa upande wake Mgeni rasmi amewataka waajiri waachane na kasumba ya kuona vyama vya wafanyakazi ni uadui baina yao na wafanyakazi walio waajiri.
Katika uchaguzi uliofanyika Mwenyekiti aliyemaliza muda wake kwa kipindi cha miaka mitano Peter Songela amechaguliwa tena kukiongoza chama hicho kwa Kanda ya Nyanda za Juu kusini.
Maeneo mengine yaliyohusisha uchaguzi kwa mujibu wa katiba yao toleo la 2011, ni Sekta ya mawasiliano kwa njia ya barua na vifurushi, Sekta ya uwakala wa kupokea kuhifadhi, kutumana kukabidhi mizigo, Sekta ya usafirishaji wa mizigo kwa njia ya barabara, Sekta ya usafirishaji mafuta kwa njia ya bomba, Sekta ya mawasiliano televisheni na Redio, Sekta ya Mawasiliano kwa njia ya simu,
Pia nafasi maalum kwa wanawake, Wajumbe wa kuwakilisha ngazi ya mkoa na mjumbe mmoja wa kuwakilisha Baraza kuu.
COTWU(T) ni kifupisho cha maneno ya kiingereza Communicationn and Transport Workers’ Union of Tanzania
No comments:
Post a Comment