Bw.Samuel Sitta
Na Anneth Kagenda
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Samuel Sitta, ametakiwa kuacha mara moja tabia yake ya kuikashfu ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na utekelezaji
wake kwa kuwa kufanya hivyo ni kuupotosha umma.
Kadhalika, Bw. Sitta ametakiwa kutoitisha mkutano wowote kwa wakazi wa Dar es Salaam hadi apate barua kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete na endapo hatapata aendelee kufanya katika mikoa mingine.
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Samuel Sitta, ametakiwa kuacha mara moja tabia yake ya kuikashfu ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na utekelezaji
wake kwa kuwa kufanya hivyo ni kuupotosha umma.
Kadhalika, Bw. Sitta ametakiwa kutoitisha mkutano wowote kwa wakazi wa Dar es Salaam hadi apate barua kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete na endapo hatapata aendelee kufanya katika mikoa mingine.
Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa CCM mkoani humo, Bw. John Guninita alipofanya ziara katika Kata ya Mbezi na Kata mpya ya Msigani kuzungumza na viongozi wa chama hicho ambapo alisema kuwa pamoja na kutoruhusiwa kufanya mkutano huo, pia Bw. Sitta aache kuleta maslahi ya kunyimwa uspika kwenye chama.
Kauli ya Bw. Guninita inashabihiana na iliyotolewa juzi na Mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Khamis Kagasheki aliyewazuia Bw. Sitta na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Bw. Nape Nnauye kufanya mkutano jimboni mwake kuhubiri siasa zao za kuvuana magamba.
Bw. Guninita alisema kuwa hivi karibuni Bw. Sitta alikaririwa kwenye mkutano wake mkoani Mbeya akisema maneno ya 'kuikashfu ilani ya CCM' huku akisema kuwa Tanzania siyo nchi maskini kama inavyoelezeka, eti serikali haijatekeleza ilani na kusema kuwa kufanya hivyo anakuwa hakitendei haki chama hicho huku akiupotosha umma wa Watanzania kwa maneno yake hayo.
'Viongozi wa namna hii tusiwavumilie hata kidogo mtu kama Waziri Sitta hawezi kukaa kwenye mkutano kama ule na kusema maneno ya namna hiyo ikizingatiwa yeye alikuwa waziri tangu enzi za hayati Mwalimu Julius Nyerere, lakini pia utaratibu wetu ni kwamba mtu akikerwa na jambo fulani anakaa kwenye vikao na kuzungumza hivyo kuzungumza maneno hayo ndiko kunakusababisha chama kishindwe kwenye chaguzi.
'Isiwe kuwa ni hasira ya kuondolewa uspika ndiyo inayo mpelekea kusema hivyo kwani kilichofanyika bungeni ni kutaka 50 kwa 50 kwamba kipindi hiki aongoze mwanamke ambaye ni Mheshimiwa Anne Makinda, hivyo aache kuleta nongwa kwenye chama, ninawaomba ndugu zangu wana CCM mpuuze Waziri Sitta kwani inaonekana ana mipango yake mingine anayoijua mwenyewe,' alisema Mwenyekiti huyo.
Alisema kuwa maneno ya Waziri huyo ni ya kukibomoa chama kwani hajatumwa na Katibu Mkuu Taifa, Bw. Wilson Mukama wala Rais Kikwete na kwamba viongozi hao hawawezi kumtuma maneno ya kubomoa serikali yao na kuuyumbisha umma kama alivyofanya.
Bw. Guninita alisema kuwa ikiwa watu wa namna hiyo wataendelea kuachwa upo uwezekano mkubwa wa kukipoteza Chama ifikapo uchaguzi wa 2014/2015 na kusema kuwa hali hiyo inasababisha upinzani kuendelea kujipanga ukiwa na matumaini kuwa wakipata urais basi watakuwa wamemaliza kila kitu.
'Huyu Bw. Sitta mimi nashindwa kumuelewa anapokaa barabarani na kusema adharani kuwa Ilani haijatekelezeka anataka tukienda viongozi tupigwe mawe kwa sababu kufanya hivyo ni kutaka wananchi watuone hatufanyi kazi yoyote ya kuwaletea maendeleo kwani CCM ndicho chama kinachotawala anaposema nchi siyo maskini anamaanisha kwamba viongozi hawawajibiki ipasavyo,' alihoji.
Akizungumzia kuhusu kujivua gamba alisema kuwa watu wamekuwa wakipotosha kuhusu neno hilo na kusema kuwa maana ya kujivua gamba ni kubadilisha tabia na wala siyo kufukuzana na kusema kuwa kufukuzana ni kukibomoa chama hicho.
'Nimekuwa nikienda sehemu mbalimbali utawasikia wanachama wakisema mvue gamba huyo katibu, hatuwezi kwenda hivyo kinachotakiwa ni kukaa kwenye vikao, kuelezana, kuelimishana na kusema ukweli mtu akionekana hakubaliani na yale anayotakiwa kufanya hatua zitachukuliwa dhidi yake lakini siyo kwamba mtu anajivua gamba anafukuzwa hata Rais Kikwete hapendi tabia hii,' alisema.
Aliwataka viongozi wa chama hicho kuhakikisha wanawajibika ikiwa ni pamoja na kuwatembelea wananchi na kujua matatizo waliyonayo na kusema kuwa kufanya hivyo ndio utakuwa muarobaini wa kukifanya chama hicho kiweze kushika dora.
Majira
No comments:
Post a Comment