Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Sunday, July 24, 2011

Precision Air yagawa tiketi za Hahaya, Comoro na Johannesburg, S.A bure

Baadhi ya washindi sita wa tiketi za Precision Air kwenda Hahaya na Johannesburg, Bi. Frida Bishota na Bw. Paritosh Bablah wakionyesha tiketi zao katika droo maalum iliyochezeshwa Mlimani City jumamosi (jana). Kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara Precision Air Bw. Phil Mwakitawa na Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa Precision Air Bi. Elizabeth Mungwe.
Mkurugenzi wa Biashara Precision Air Bw. Phil Mwakitawa (Kulia) akimzawadia mshindi wa tiketi (kwenda na kurudi) ya Johannesburg, S.A., Bw. Paritosh Bablah baada ya droo maalum ilichezeshwa Mlimani City
Mkurugenzi wa Biashara Precision Air Bw. Phil Mwakitawa (Kulia) akimzawadia mshindi wa tiketi (kwenda na kurudi) ya Hahaya, Comoro Bi. Frida Bishota baada ya droo maalum iliyochezeshwa Mlimani City jumamosi (jana).
Maofisa wa Idara ya Masoko na Mauzo Precision Air wakimtaarifu kwa simu mmoja wa washindi wa promosheni ya kwenda Hahaya, Comoro na Johannesburg, S.A.
Ofisa Masoko na Mauzo wa Precision Air Bi. Yvonne Baldwin akitangaza jina la mmoja ya washindi wa droo maalum za tiketi kwenda Hahaya, Comoro na Johannseburg S.A., iliyofanyika Mlimani City jumamosi (jana). Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano Precision Air, Bi. Elizabeth Mungwe na Mkurugenzi wa Mtandao na Mipango Precision Air Bw. Patrick Ndekana.

No comments: