Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, July 26, 2011

MZEE ERNEST PAULO WAYA ASEMA SERIKALI IACHE TABIA YA KUWAONA WAMAANA WAKATI WA SIKU YA MASHUJAA IWAJALI MUDA WOTE

Mzee Ernest Paulo Waya  aliyepigana vita kuu ya pili vya Dunia  akiongea na Mbeya Yetu  amesema serikali imewatelekeza na kutowajali kwa chochote na kuwazulumu mafao yao mashujaa hao wa zamani ila huwaona wamaana sana siku ya mashujaa na kuwaita ili washiriki pamoja siku hiyo zoezi hilo likiisha huwatelekeza mpaka mwaka mwingine tena mzee Waya amesema ndiyo maana mwaka huu wenzake wengi hawajaja wapo kujitafutia riziki maana kula yao niyashida sana
Mzee Ernest Waya akiweka upinde na mshale kuwakumbuka wenzake aliokuanao vitani enzi hizo
Mzee Ernest Waya akitoa heshima mara baada ya kuweka upinde na mshale
Toka kushoto ni Mkuu wa Mkoa Mbeya John Mwakipesile wapili ni Mstahiki meya wajiji la  Mbeya  Mh Atanas Kapunga watatu Mzee Ernest Waya wanne ni mwakilishi wa machifu wa Mbeya
Shughuli imekwisha Mzee Waya huyoo ndiyo wamekwisha msahau hawana mpangonae tena
Hapa anaelekea ofisi ya mkuu wa Mkoa Mbeya apate msaada wa usafiri kumrudisha kwake Mbalizi
JAMANI TUWAJALI WAZEE WETU

No comments: