Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, July 11, 2011

JUST IN: MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AZINDUA KUMBUKUMBU YA KIGODA CHA MWL NYERERE

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kumbukumbu ya Kigoda cha Mwalimu Nyerere kinachohusika na masuala ya Mazingira na mabadiliko ya Tabianchi, kilichozinduliwa leo Julai 11, 2011 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kutangazwa kwa Mwenyekiti wa kwanza wa Kigoda hicho,  Prof. Pius Yanda. Picha na Muhidin Sufiani-OMR 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpongeza Prof. Pius Yanda, baada ya kutangazwa na kuvishwa Joho la kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa Kigoda cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kigoda hicho uliofanyika leo Julai 11, 2011 katika ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani
Baadhi ya Mabalozi wa nchi za nje nchini Tanzania, waliohudhulia hafla hiyo ya uzinduzi wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere.
Baadhi ya washiriki katika hafla hiyo ya uzinduzi wa kigoda cha Mwalimu Nyerere.
Baadhi ya wageni waalikwa na Mabalozi waliohudhuria hafla hiyo ya uzinduzi.
Mkurugenzi na Kiongozi wa Bendi ya Mjomba, Mrisho Mpoto, akiigiza kusafiri na Ngamia wake, wakati akitoa burudani ya kuimba mbele ya mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere kilichozinduliwa leo Julai 11, 2011 Chuo Kikuu Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Wasanii wa Bendi ya Mjomba, wakishambulia jukwaa wakati wakitoa burudani kwenye hafla ya uzinduzi wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere, uliofanyika leo Julai 11, 2011 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Prof. Amos Majule (kulia) kuhusu vijitabu vya kumbukumbu, wakati akikagua vitabu hivyo baada ya kuzindua Kigoda cha Mwalimu Nyerere. Uzinduzi huo ulifanyika leo Julai 11, 2011 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Kigoda cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, kilichozinduliwa leo.

 




No comments: