Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Sunday, June 19, 2011

RAIS KIKWETE ZIARANI SEYCHELLES


Rais Jakaya Kikwete akipokewa rasmi na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Seychelles Mheshimiwa James Alix Michel mara tu baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa Victoria nchini humo tarehe 18.6.2011 kwa ziara ya kikazi ya siku moja.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa na Mke wa Rais wa Seychelles Mama Natalie Michel kwenye uwanja wa mpira mjini Victoria wakati wa sherehe za kuadhimisha sikukuu ya taifa hilo tarehe 18.6.2011.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Rais Mstaafu wa Seychelles Mheshimiwa James Manchan kwenye uwanja wa mpira wa mjini Victoria,mji mkuu wa Seychelles wakati wa kuadhimisha sherehe za siku ya Taifa hilo tarehe 18.6.2011.
Vijana wa chipukizi wakitoa heshima kwa mgeni rasmi wakati wakipita mbele yake wakati wa maadhimisho ya siku ya taifa ya nchi hiyo tarehe 18.6.2011.
Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Seychelles Mheshimiwa James Michel kweye ikulu ya nchi hiyo mjini Victoria tarehe 18.6.2011
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika mazungumzo na Mke wa Rais wa Seychelles Mama Natalie Michel huko ikulu tarehe 18.6.2011
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na Natalie Michel mke wa Rais wa nchi hiyo kwenye ikulu ya nchi hiyo mjini Victoria tarehe 18.6.2011.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na Rais James Michel kwenye ikulu ya nchi hiyo mjini Victoria tarehe 18.6.2011.(Picha zote na John Lukuwi)

No comments: