Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, June 1, 2011

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA, SONGEA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa zinduzi wa Sherehe za maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani, zinazofanyika kitaifa mjini Songea Mkoani Ruvuma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akibonyeza kitufe kuashiria kuzindua rasmi maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani yanayofanyika kitaifa mjini Songea mkoani Ruvuma. Sherehe hizo zimeanza leo Juni 01, katika Uwanja wa Majimaji. Kulia ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Zakia Bilal na (katikati) ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Christine Ishengoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea Moa wa Ruvuma kwa ajili ya kuzindua rasmi sherehe za maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, DKt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma ujumbe kuhusu zoezi la kuzuia uchomaji wa misitu katika mabango yaliyokuwa yameshikwa na vijana, wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonyesho katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, zilizozinduliwa leo Juni 01 kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea Mkoa wa Ruvuma. Kulia ni mkewe Mama Zakia Bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Asasi isiyo ya Kiserikali ya Mkoa wa Ruvuma, Methord John, kuhusu uzalishaji wa matofali yanayochomwa kwa kutumia Makaa yam awe, wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonyesho katika sherehe za uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani zilizoanza mjini Songea mkoa wa Ruvuma leo Juni 01, kwenye Uwanja wa Majimaji.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya wasichana ya Songea (Songea Girls) wakiwa ni miongoni mwa waliohudhuria sherehe hizo za maadhimisho kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea Mkoa wa Ruvuma leo Juni 01.
Picha zote na Muhidin Sufiani wa OMR

No comments: