Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, May 26, 2011

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA 6 WA KIMATAIFA WA MAWASILIANO ICT

Makamu wa Rais akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya watu waliopresent paper zao.

Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihojiwa na waandishi wa habari baada ya kufungua mkutano huo wa sita wa Kimataifa wa Afrika kuhusu Teknolojia ya Taarifa na Mawasiliano ya Ustawi, Elimu na Mafunzo (ICT), uliofunguliwa jijini Dar es Salaam jana Mei 25.

Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Samwel Muro, wakati alipotembelea banda lao la maonyesho baada ya kufungua mkutano wa sita wa Kimataifa wa Afrika kuhusu Teknolojia ya Taarifa na Mawasiliano ya Ustawi, Elimu na Mafunzo (ICT), uliofunguliwa jijini Dar es Salaam jana Mei 25.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, akijaribu kuvaa miwani ili kuweza kuona picha iliyokuwa ikionyeshwa ukutani kupitia Screen na Projector (Animation Fils) , wakati alipotembelea Banda la maonyesho baada ya kufungua mkutano wa sita wa Kimataifa wa Afrika kuhusu Teknolojia ya Taarifa na Mawasiliano ya Ustawi, Elimu na Mafunzo (ICT), uliofunguliwa kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam jana Mei 25. Kushoto ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka na Waziri wa Elimu na Mafunzo, Shukuru Kawambwa (kulia) ni Mkurugenzi wa Designmate Animation Films, Colonel Basavaraj
Prof Tibaijuka naye akijaribu miwani hiyo ili kuona picha hiyo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Imelda Lutebinga na Langton Chibura wakati alipotembelea Banda lao la maonyesho la SEACOM Tanzania Ltd, baada ya kufungua mkutano wa sita wa Kimataifa wa Afrika kuhusu Teknolojia ya Taarifa na Mawasiliano ya Ustawi, Elimu na Mafunzo (ICT), uliofunguliwa jijini Dar es Salaam jana Mei 25

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipongezwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, baada ya kufungua mkutano wa sita wa Kimataifa wa Afrika kuhusu Teknolojia ya Taarifa na Mawasiliano ya Ustawi, Elimu na Mafunzo (ICT), uliofunguliwa jijini Dar es Salaam jana Mei 25

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akifungua rasmi mkutano wa sita wa Kimataifa wa Afrika kuhusu Teknolojia ya Taarifa na Mawasiliano ya Ustawi, Elimu na Mafunzo (ICT), uliofunguliwa jijini Dar es Salaam jana Mei 25.

Waziri wa Elimu wa na Mafunzo ya Ufundi, Shukuru Kawambwa, akizungumza baada ya makamu wa rais kufungua mkutano huo.
Baadhi ya Mawaziri na Manaibu wao waliohudhuria ufunguzi wa mkutano huo, wakifuatilia maonyesho ya picha zilizokuwa zikionyeshwa katika Screen za ukutani.
Mawaziri wakipiga makofi kumpongeza Makamu wa Rais baada ya kumaliza hotuba yake.
Wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye mkutano huo hapo jana.

No comments: