Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Saturday, May 21, 2011

Dk Bilal aongoza mazishi ya Mwenyekiti wa Wazee wa CCM Dar es salaam

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka mchanga kwenye kaburi la aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Athumani Hassan Mwinyimvua, aliyefariki dunia na kuzikwa jana Mei 20 kwenye Makaburi ya Karume Mwembechai.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihudhuria maziko ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Athumani Hassan Mwinyimvua, Makaburi ya Karume Mwembechai.
Waumini wa Dini ya kiislamu wakibeba jeneza lenye mwili wa marehemu, Athuman Hassan Mwinyimvua, baada swala ya mwisho iliyofanyika katika Msikiti wa Mwembechai Dar es Salaam na kuzikwa katika makaburi ya Karume Mwembechai jijini


Wanachma wa CCM na wakaazi wa jijini Dar es Salaam, wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa marehemu Athuman Hassan Mwinyimvua, aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Hayati Mwinyimvua Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi Ya Makamu wa Rais

No comments: