Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Saturday, May 21, 2011

BONANZA LA WAFANYAKAZI WA PASADA LAFANA LEO HII

Hapa wafanyakazi wa Pasada wakiweka viungo vya mwili sawa kabla ya kuanza kwa Bonanza 

Hapa Mkuu wa Idara ya Fedha Mr. Eliawony Makatta ambae ndo alikua mgeni rasmi akifungua Bonanza rasmi.

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Mr. Chiziza akisema maneno machache ya kuwakaribisha wafanyakazi wa Pasada kwenye Bonanza

Mbio za magunia ni moja ya michezo iliyofana kwenye bonanza hilo washiriki wakiwa wanatoka idara tofauti tofauti za Pasada


Mchezo wa kukimbiza kuku nao ulikuepo, hapa Mr Haule, Fikiri na wengine wakimkimbiza kuku huyo kwani waliacha maji yakichemka majumbani.

Fikiri Mdegela ndo aliibuka kidedea wa kumdaka kuku huyo na kupata kitoweo cha siku hiyo.

Wamama wafanyakazi wa Pasada nao hawakua nyuma kwani na kuku wao alikuepo, hawa wanafanya kazi katika idara tofauti tofauti ilikua vizuri kwao kwani ni mara chache kuwa pamoja kama hivi.

Wazee wa Pasada nao hawakusahaulika hapa ni Mr. Chiziza, Mr. Fabian Malya wakimgombania kuku aliyekimbizwa na wazee. Mr Malya ( Blue) ndio aliibuka mshindi na kuondoka na kuku huyo.

Kandanda nayo ilikuepo hapa ni kati ya timu ya idara ya Fedha na utawala pamoja wakipambana na idara ya medical, na mwenye mpira ni Dr. Alick Kayange.

Wakiwa mapumziko huku wengine wakiwa wameshika viuno kuashiria kuchoka sana, waliokaa ni Dr. Chiduo, Dr. Mchelle Mchelle, Dr Alick na mwenye njano ni meneja mwajiri Mr. Leonard Richard

Mlinda mlango wa timu ya utawala na fedha Mr. Sillah Mbuya akimtoka Dr Marwa wa medical mwenye fulana nyekundu.

Mshangiliaji namba moja mama Minja akiwa analipuliza vuvuzela kwa nguvu zote huyu anatoka idara ya medical.

Kikosi cha idara ya ushauri pamoja na huduma majumbani kwenye picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo wa mpira wa miguu.


Huyu ndio mlinda mlango wa timu hiyo ya idara ya ushauri na kupima, hii staili ni mpya ya mlinda mlango kuvaa dela.

Idara ya watoto na Kifua kikuu wakishangilia ushindi kwa staili yake baada ya kuwafunga idara ya ushauri na huduma majumbani



Meneja mwajiri Mr. Leonard Richard akimkaribisha mgeni rasmi kukabidhi zawadi kwa washindi wa siku hiyo ya bonanza.

Baada ya shughuli zote hapa wafanyakazi wa Pasada wakipata chakula cha mchana kwa pamoja.

No comments: