Katuni ya leo, kama ilivyowasilishwa na msanii wa uchoraji Said Michael
Msanii wa uchoraji Said Michael, ametoa mtizamo wake kuhusiana na hali inavyoendelea kule nchini Libya ambako majeshi ya wakubwa, yakiongozwa na vikosi vya Wamarekani yameweka kambi kule yakimuadabisha mtawala wa nchi hiyo kanali Muammar Gaddafi anachoonyesha ni kile ambacho kiko vichwani mwa watu wengi ndani ya bara letu la Afrika. Kwamba ni kwanini AU (Umoja wa nchi za Afrika), umekaa kimya ukiangalia tu yanayoendelea Libya kana kwamba nchi hiyo sio sehemu ya wanachama wake? Habari kwa hisani ya jukwaa huru media
No comments:
Post a Comment