Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, April 28, 2011

IRANI YATOA DOLA MILIONI 1.2 KUSAIDIA KILIMO KWANZA NCHINI

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu (Kulia),akizungumza na Naibu Balozi wa Irani hapa nchini Bw Bahman Ahmadi(Kushoto) alipomtembelea Ofisini kwake leo. Mwingine ni Mshauri wa kibiashara katika Ubalozi wa Iran hapa nchini Bw Mobasher.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu (Kushoto),katika picha ya pamoja na wageni wake Naibu Balozi wa Irani hapa nchini Bw Bahman Ahmadi(Katikati) na Mshauri wa kibiashara katika Ubalozi wa Iran hapa nchini Bw Mobasher (Kulia).


Katika kusaidia kutekeleza kwa vitendo kampeni ya Kilimo Kwanza, Serikali ya Irani itaisadia Tanzania Dola za kimarekani Milioni moja pointi mbili ($ 1.2Mil) kwa ajili ya kampeni hiyo.

Taarifa hiyo njema imetolewa Jijini Dar es salaam leo, wakati Balozi Msaidizi wa Iran hapa nchini Bw Bahman Ahmadi alipotembelea Wizara ya Viwanda na Biashara na kukutana na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mh Lazaro Nyalandu.

Katika mazungumzo hayo yaliyojikita katika kuimarisha Uhusiano mwema bana ya nchi hizi mbili hasa kibiashara, Mh Nyalandu kwa niaba ya serikali ya Tanzania, ameishukuru serikali ya Iran kwa msaada huo na kuahidi kuwa utatumika kama ulivyokusudiwa.

Aidha, Mheshimiwa Nyalandu amewakaribisha wawekezaji kutoka Iran kuja nchini na kushirikiana na wazalendo katika kutumia vyema fursa mbalimbali zilizopo hasa katika sekta ya Kilimo.
Habari kwa Hisani ya Michuzi Blog

No comments: