Mmoja wa watoa mada juu ya taratibu za kituo cha uwekezaji nchini TIC ambaye pia ni afisa elimu kwa umma bwana John Mnali akiwasilisha mada yake
Mfanyabiashara mkubwa wilayani Mbozi Unyiha Associate bwana Charles Chenza akitoa malalamiko juu ya namna vibali vya msamaha wa kodi visivyowasaidia wawekezaji wadogo na badala yake kuwanufaisha wafanyabiashara wakubwa nchini kutokana na mlolongo na urasimu wa kupatikana kibali hicho
Sehemu ya mabango yanayozungumzia shughuli za TIC nchini Tanzania
Kazi ilianzia hapa baada ya Meneja wa Kanda wa kituo cha Uwekezaji alipoamua kupasua jipu hadhani kuwa "TIC na TRA vyote ni vyombo vya serikali, lakini hapa naomba nieleze wazi kuwa TRA imekuwa ikiwaona wafanyabiashara wa mkoa wa mbeya kama wakwepa kodi na hawaaminiki!!!, nimekuwa nikipokea malalamiko kila siku meengi yakiihusu TRA kuwanyanyasa wafanyabisahara, na hali hii nimeiona ni tofauti na mikoa mingine kama ARUSHA, DAR na Mwanza, sasa sijui TRA Mbeya wapo makini hata kuliko Pale ambako kamishna wa kodi yupo (DAR ES SALAAM) hebu tuwatendee haki wawekezaji manake tukifanya hivi tunadumaza uwekezaji mkoani mbeya.
No comments:
Post a Comment