Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, March 14, 2011

MTINANGE HUKO IRINGA TIMU YA TIMU YA WAANDISHI WA HABARI YAIADHIBU TANESCO IRINGA 2-1

Mgeni Rasmi akisalimia wachezaji Muda mchache kabla ya mtinange 

Timu hiyo ya waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali ambao wanaunda timu ya chama cha waandishi wa habari za michezo Tanzania (TASWA ) mkoa wa Iringa ikiongozwa na mwenyekiti wake Francis Godwin leo imeweza kufanya vema katika mashindano hayo ya kombe la maji baada ya kuiadhibu kwa jumla ya goli 2-1 timu ya Dowans (Tanesco) Iringa.
Mchezo huo ambao ulikuwa mzito kwa timu zote mbili ambapo zilionyesha kukamiana kupita kiasi ,Timu ya waandishi wa habari iliweza kumudu vigingi vya wana Dowans Tanesco Iringa bila kujali madhara ya kukatiwa umeme baada ya kuiadhibu goli la kwanza mapema dakika ya 24 kipindi cha kwanza .
Kama haitoshi mchezaji wa kutoka kicho cha radio Ebony Fm Emanuel Nyeho alipata kuiongezea goli la pili timu hiyo ya waandishi wa habari kupitia mkwaju wa peneti .
Hadi timu zote mbili zinakwenda mapumziko Tanesco walikuwa bado hawajapata goli lolote huku wanahabari wakiwa mbele kwa goli 2
Kipindi cha pili Tanesco waliongeza mashambulizi zaidi na kujipatia goli la kufutia machozi japo hadi mchezo unamalizika wanahabari kutoka Ebony Fm,Country FM , Overcomers Fm ,Qbla Teni ,IMTV na wale wa magazeti ya Tanzania daima na Mtanzania na NIpashe walikuwa wakitoka nje ya uwanja huo wakiwa na uhakika wa kusonga mbele katika mashindano hayo huku Tanesco wakikabidhiwa rungu la kuendelea kusoma mita.
Akizungumza katika michezo hiyo Mhe. Ndaki ambaye alimwakilisha mstahiki meya wa Manispaa ya Iringa alitaka wachezaji hao kuendeleza michezo hiyo kwa amani zaidi na kuwa ili kuhamasisha michezo zaidi waandaaji wa mashindano hayo Iruwasa wameshauriwa kupanua wigo zaidi kwa kuongeza timu nyingi zaidi.
Mashindano hayo ambayo yanaendelea katika uwanja wa sekondari ya Lugalo ni timu nane ndizo zinazoshiriki ambapo hadi sasa tayari timu tatu zimeaga mashindano hayo ikiwemo timu ya Halmashauri ,Madereva Tax na Tanesco Iringa huku timu ambazo zinaendelea na mashindano hayo ni Waandishi wa habari ambao jumapili watapambana na waandaaji wa mashindano hayo Maji .
Hata hivyo tim kali zilizosalia ni VETA , RAS ,MAJI na VETERANI ambazo wanahabari hao wamedai si lolote kwao.
Kutokana na ushindi huo timu hiyo ya waandishi wa habari ambayo inagombea kombe la shilingi 250,000 litakalo tolewa kwa mshindi wa kwanza na mshindi wa pili 150,000 ,kwa sasa imetangaza siku za mazoezi katika uwanja wa chuo cha Mkwawa mazoezi yatakayoanza siku ya jumatano jioni

No comments: