Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, March 7, 2011

MCH. MWASAPILE NA DAWA YA MUGARIGA LOLIONDO

Misururu ya magari mbalimbali iliyoleta wagonjwa na wasio wagonjwa kwenda kunywa dawa ya Mugariga katika kijiji cha Samunge wilayani Loliondo, aliyooteshwa na Mzee Mwasapile mwaka 1991. 


Picha kwa hisani ya Aman Masue
Mchungaji Ambikile Mwasapile akitoa dawa kwa wagonjwa wake




Muhtasari wa dawa na Tabibu:


  1. Mgunduzi wa dawa ni Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwasapile (76) anayesema alioteshwa ndotoni na Mungu tangu mwaka 1991 ili aitumie kutibu watu
  2. Mahali anakopatikana ni eneo la kwa Mchungaji katika Kijiji cha Samunge, Sale, wilayani Ngorongoro, umbali ya takriban kilometa 400 kutoka jijini Arusha.
  3. Jina la dawa ni "Mugariga" inatokana na mti aina ya mugariga.
  4. Matumizi yake ni kunywa kikombe kimoja tu, na ni marufuku kurudia.
  5. Gharama yake hadi sasa ni shilingi 500/- tu.
  6. Mchungaji anasema dawa inatibu maradhi sugu kama vile UKIMWI, kisukari, pumu, saratani n.k.
  7. Watu wamekuwa wakifika Samunge kwa njia mbalimbali, binafsi na hata za kutumia vyombo vya serikali. Wengine hutembea kwa miguu, kukodi magari (kukodi gari kutoka jijini Arusha itakugharimu kati ya shilingi 80,000 na 100,000 il hali mabasi ya kawaida yakitoza kati ya sh. 40,000 na 65,000.), pikipiki, helikopta na magari ya Serikali (kama inavyoonekana pichani).
  8. Wingi wa watu, kuanzia juzi (Ijumaa) umesababisha askari wa Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakishirikiana na mgambo kuweka ulinzi kulinda usalama na kuhakikisha watu wanapata dawa bila kutokea vurugu.
  9. Msaidizi wa Mch. Mwasapile, Marko Nedula amesema tayari Askofu wa KKKT jimbo la Arusha, Thomas Lazier aliwatembelea na kuahidi kusaidia upanuzi wa eneo la kutolea dawa.

No comments: