UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umeitaka sekretarieti ya chama hicho kujizulu kabla umoja huo
haujachukua hatua za kuwaondoa kwa kuwa imeshindwa kumsaidia Rais Jakaya Kikwete.
haujachukua hatua za kuwaondoa kwa kuwa imeshindwa kumsaidia Rais Jakaya Kikwete.
Akifungua Baraza la Umoja wa Vijana Mkoa wa Pwani jana, Makamu Mwenyekiti wa umoja huo wa mkoani humo, Bw. Abdallah Ulega alisema kuwa sekretaeti hiyo haifai kwa kuwa ilisababisha chama hicho kushinda kwa taabu katika uchaguzi mkuu uliopita.
“Katika uchaguzi uliopita tulishinda kwa kupata asilimia 61 ya kura zilizopigwa ukilinganisha na mwaka 2005, ukijiuliza ni kweli CCM imepoteza imani kwa wananchi kwa kiasi hicho jibu linakuja kuwa sekretarieti haikuwajibika ipasavyo, hivyo tunasema kama wamechoka waondoke kama hawataondoka lazima waondolewe hawafai,” alisema Bw Ulega.
Alisema kuwa watu walimo katika sekretarieti hiyo ndiyo wanatoa siri kwa Chama cha Demkrasia na Maendeleo (CHADEMA) na imeshindwa kumshauri na kumtetea rais katika mambo mengi ya msingi hadi anaposimama na kujitetea mwenyewe.
Mkutano huo ulihudhuliwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa na wenyeviti umoja huo kutoka katika Mikoa ya Kagera, Lindi Kigoma, wabunge kadhaa na Mjumbe wa Baraza la Utekelezaji la jumuiya hiyo, Bw. Ridhiwan Kikwete.
Secreterieti inayoongozwa na Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusuf Makamba, inajumuisha Manaibu Katibu Wakuu Bara, Kapteni George Mkuchika na Salehe Ramadhani Ferouz (Zanzibar), Katibu wa Itikadi na Uenenezi, Kapteni John Chiligati, Katibu wa Idara ya Uchumi na Fedha, Bw. Amos Makala na Katibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe.
Mbalio na sekreterieti hiyo, Bw. Ulega alisema kuwa watu wengi walio katika serikali wanatakiwa kujibu hoja za dhidi ya serikali akutokana na vitengo vyao na si lazima wasubiri Rais Kikwete kujibu hoja hizo.
“Kuna watu wa kujibu hoja, katika mfumuko wa bei yuko gavana na watu wa kumsaidia amewekewa, kuna naibu gavana na wakurugenzi wengine, shughuli yake ni kujibu hoja ya mfumuko wa bei lakini anainuka rais na kujibu hoja hiyo wao wanafanya nini.
“Labda watuambie kama wanamilikiwa na bwana wengine na kumuacha rais akihangaika pekee yake, naomba niseme tena bila kumung’unya, kama wanahisi hawezi kazi wakae pembeni na kama wanatumukia mabwana wawili watachanika msamba,” alisema Bw. Ulega.
Alisema ni kitendo cha kushangaza kwa Mawaziri Wakuu Wastaafu, Bw. Edward Lowassa na Bw. Fredrick Sumaye kushindwa kukutana na rais na kumpa ushauri, na kukimblia katika magazeti na kutoa shutma.
“Hawa watu ni mwaziri wakuu wastaafu, wanaweza kufanya ahadi kwa dakika 30 tu wakaonana na rais lakini wanakimbilia katika magazeti na kutoa kauli zinazohatarisha amani na kukivuruga chama,” alisema.
Alisema Bw. Lowassa ni Waziri Mkuu mstaafu, mbunge na mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, alipaswa kuwa mwangalifu katika kauli zake anazotoa hususani kutaka mishahara ipande huku akijua kuwa hali ya uchumi si nzuri.
Bw. Ulega alisema kauli hizo zimelenga kutaka urais mwaka 2015, jambo ambalo kwa sasa wamechelewa kwa kuwa liko mikononi mwa mwenyekiti wa chama, Rais Jakaya Kikwete kuwa kuwa ndiye anayemjua rais wa 2015.
Alisema viongozi hao wameacha utaratibu mzuri wa chama hicho kutoa maoni yao kupitia vikao na kutoa shutuma zao kupitia magazeti wakidhani wanakikomoa chama, nchi itaendelea kusonga mbele na kuwapa pole wale wanaodhani rais lazima atoke kaskazini.
“Kama wanataka urais wasubiri muda wachuke fomu na kuwashawishi wajumbe wawachague lakini kwa kumtukana mwenyekiti hawatapata kamwe kwa kuwa yeye ndiye anayejua ni nani muadilifu, hivyo wasiharibu nchi kwa maslahi yao. Wao wameshiba na sasa wamevimbiwa watauache na sisi tule kama wao.
“Mimi nasema hapa simung’unyi maneno tuziogope sana fedha zao, mimi sijala hata shilingi moja ya mtu na sihitaji kufanya hivyo,” alisema.
No comments:
Post a Comment