Hiki kinajieleza chenyewe
Hii ni Hotel ya Matema Beach resort ipo Mjini Kyela.. pindi ukianza tuu safari ya kuingia mji huo
Huu ni mto Songwe moja ya mto mkubwa unatoka Malawi unakatiza Tanzania kuelekea pande za Zambia
Hii ni bara bara kuu inayo elekea katika boda ya Malawi na Tanzania
Hapa ni eneo ambalo kuna maduka mengi na wafanya biashara wengi wanapatikana eneo hili hapa. ukitaka mchele bora, pia samaki wa kutoka ziwa Nyasa
Pia ni aina ingine ya usafiri lakin apa ndio mwisho wa kituo kabla haujaingia barabara kuu inayo elekea boda la Tanzania na Malawi
Huu ndio usafiri unaotumika kwenda huko interior kyela kufika maeneo kama ya Ipinda na mengineyo na hiyo
ndio bara bara kuu kuelekea Matema Beach
Huko kijijini pia mitumba bei poa kama inavyo onekana apo kwa uzuri kabisa
Swala zima la elimu wilayani Kyela pia haliko nyuma ule mpango wa Serikari kujenga shule bora umeboreshwa kama unavyo kiona hicho kibao cha shule pia madarasa yako hivyo na walimu wenye bidii ya kufundisha na wanafunzi smart.
Hii ni jadi kwa watalii na wadau wengi wanapotoka Kyela matema Beach hupendelea kununua samaki na kuwatunduka kwa gari kama inavyo onekana apo ikiwa ni kama alama kuwa walikua Kyela
Baadhi ya wadau wakiwa vakasheni Matema Beach Kyela
Huu ni mtumbwi wa aina yake unatumika kuzungusha watalii ndani ya ziwa nyasa pindi wanapo kuja vakashen
Haya ni mawe mazuri ambayo yako ndani ya ziwa Nyasa, ukitembelea usikose kuchukua ili ukapambe kwako
Huu ndio muonekano wa Matema Beach kwa Umbali mchanga mwanana na ziwa kwa pembeni
Huu ni mwanzo tuu wa kuwaletea mambo yapi yanajili katika wilaya ipi Jijini Mbeya endelea kuwepo kujua ni Eneo gani litafuatia.ukiwa unataswila la eneo lolote Mkoani Mbeya pia usisite kututumia kwa mbeyayetu@yahoo.com
No comments:
Post a Comment