Bara bara ya kuelekea kwa Babu
Ngorongoro hapa
Oldoinyo Lengai huko njiani
Huduma ya misosi karibu na kwa babu
Huduma zinginezo kwa Babu
Hapa ni nini sijui, kama mita mia kabla ya kikombe
Hiyo nyumba ya udongo nyuma ya mtu ndo kwa babu hapo
Uchavuzi wa mazingira uliokithiri kwa Babu
Mdau ameanza na kusema "Shida kubwa niliyoiona kule ni hali ya uchafuzi wa mazingira, kwani for about seven PLUS kilometres ni eneo lenye foleni hivyo kuna uchafu mwingi kama unavyoweza ona kwenye some pics, plastic za maji ya kunywa na mifuko ni mi ngi mno". Kwa eneo hilo vichaka vimejaa kinyesi na upepo ukivuma tu, harufu inakufikia popote ulipo. Hatari ya magonjwa ya mlipuko is a fact na si siasa.Halmashauri wanatoza sh 2,000 kwa gari kwa ajili ya usafi nahisi haitoshi na kazi hiyo bado. Nafikiri ingekuwa walau elfu kumi na kazi ifanyike kweli kwani eneo linalokaa watu all the time wakiwa kwenye movement za foleni ni kweli linafika km 10 na may be sometimes ni zaidi so you can imagine hali ikoje. Bahati mbaya sana mvua zinanyesha hivyo usafi wa mazingira ni muhimu zaidi.
Umbali wakufika kwa babu kutoka Arusha ni km 295+- depending on your starting point. Utatembe km 105 through monduli to Mto wa mbu, hiyo ni very smooth barabara ya lami. Then mto wa mbu kuna petro station kama mbili hapo mojawapo iko kama km 0.5 beyond the turning to babu's village (manake utarudinyuma). This is Njake petrol station na uzuri wana jenereta compared to the one before junction to Babu's village. So get your tank FULL hapo kwani unaanza km 190 za rough road ambapo utaenda (mimi) about 30km per hr. Kwenyebaadhi ya maeneo you can go up to 60 - 80 km/hr speed depending on your driving speed (note that I am slightly aheaad of an average driver in terms of uangalifu).safari from mto wa mbu tu Samange kwa babu ni kama masaa saba+- kwa kwenda na may be fewer on return as you will have idea ya hali ya barabara. Depending on consumption ya gari yako na other factors, my full tank which is 80ltrs got me kwa babu, foleni na kurudi mpaka arusha nikiwa na robo tank (sikuwasha a/c na gari liliwashwa only panapokuwa na movement).
Having said the above,Hali ya barabara si mbaya saaaana kama pakiwa pakavu,ni njia yenye mawe na some places vumbi. Sehemu korofi si nyingi sana ila kuna a lot of seasonal river or call them valleys ambazo hazina madaraja na unaweza kupita sasa hivi baaadae ukakuta pamekuwa mto size ya ruaha na bahati mbaya mvua zimeanza (zinanyesha)!!! But cha kutia moyo ni kwamba njia hiyo iko busy masaa 24 na always vijana wa Arusha na land cruiser zao za porini watakusaidia na wanajua wapi pa kuanzisha njia nyingine within the pori. 'very interesting'.
May be it is also advisable kuhakikisha kuwa uko karibu na magari mengine in case of a mechanical problem au kupotea njia hasa sehemu za seasonal rivers earlier mentioned ambapo hakuna barabara rasmi! kingine kizuri ni kiwa all along the road, utakuta makundi ya wamasa wakichunga, ni sehemu chache sana utaenda 2km bila kukuta watu. Wamasai wako so friendly na watakuomba vitu vidogo dogo kama maji, hela etc, consider giving them especially wakati wa kurudi, ni upendo mkuu kwa watu hao wenye upendo kwako.
Kwa chakula, hali si mbaya kiviiile,Misosi inapatikana na si kwa bei mbaya sana. Lakini kwa ushauri, ni vyema kubeba mikate na biskuti (snacks) pamoja na maji/soda/juice za kutosha ili kuepuka kubanwa na haja kubwa so that you can as much as possible limit your visits to pori to a fewer rounds tena mostly za haja ndogo.
Maji ya kunywa yanapatikana huko manake wafanyabishara wachache wakubwa wameweka kambi huko, Kilimanjaro ya lita 1.5 ni sh 1,500 unless hali ikibadilika. Hautashangaa kwamba hata bia, red bull, Malta etc zipo kwa bei za kawaida +- Tzs.1,500 or around that number. Mikate ndo lazima ubebe. Mama ntiliewa arusha na moshi pia wamehamia huko wanafanya mambos! 'so entreprising'!
Ushauri: ukienda huko kuwa mfano kwa kutunza mazingira na wengine wakuige ili kutunza mazingira na kuwezesha wanadamu wengine wengi kwenda huko kwa usalama.
Babu anasisitiza kwamba tuwataarifu na kuwahimiza watanzania wenzetu wanaohitaji huduma yake waende sasa, kwani kwa maono yake, the whole world is coming na itakuwa ni jambo la kushangaza kama wewe M - Tz utaenda huko wakati hali itapokuwa ni kusubiri mwezi mmoja au zaidi kupata 'kikombe', wakati nisasa. Foleni iliyopo sasa anasema 'is just like a drop of water' huko mbeleni.
Kwa kweli huduma yake ni kwa wote, haina dini wala dhehebu ni imani yako tu. Hata uendapo hapo kwenye maombi yake asubuhi, anaomba generally na salamu yake ni Habari za.... Wala si bwana asi..... Tumsifu..... Wala nini!! Na huko wako maustadhi, pagans, wakristu wa kila namna, waafrika, wahindi na kadhalika. Kwa kweli ndipo utakapogundua kwamba watu tuna matatizo mengi usione tunatembea.
Babu anasema dawa yake inatibu magonjwa sugu, cha msingi wewe unapoenda ujue unashida ipi! Kwa wenye virusi vya ukimwi anasema waende kupima baada ya siku saba, magonjwa mengine sugu ambayo ni commom kama sukari, moyo etc, hayo hupona mara moja.
So kwa anayehitaji ajipange, na kwa kweli it is part of life time event na ni adventure kwanza kushuhudia maelfu ya watu waliopo pale, marafiki unaowa pata while in queue, simple life ya huyu mtu (babu), na lingine ambalo wengi hatulifahamu kuona pundamilia wakila just aside ng'ombe wa wamasai na mma sai akichunga bila kuogopa au kuogopwa. Hawa watu (masais) ni watu pori hasa. Na uhakika mimi ningeshuka pundamilia wote wangekimbia lakini mmasai anatambulika kama mmoja wao. Pia utapita karibu na ziwa Eyasi na very close to lake Natron kwenye magadi. Kwa kweli ni safari nzuri na it is so funny, ukienda na kurudi salama. This is what I want to share nanyi may be the flow is not very good manake nimeandika sana but those are facts for your information/action !!!
Mengineyo...... tusubiri.
Habari hii imeletwa kwenu na Mdau wa kutoka Loliondo
No comments:
Post a Comment