Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Sunday, March 13, 2011

B'Hits Nominations For Tanzania Music Awards


Kwa mara nyingine muda umefika wa kuwaenzi wale wasanii mahiri waliofanya vizuri na kupata mafanikio zaidi katika mwaka ulipita. Kama kawaida kuna wasanii walioweza kuingia mara nyingi zaidi, nyimbo zilizoingia mara nyingi zaidi na pia kuna kitu ambacho wananchi wengi wamekua wakikisahau kabisa kwamba kuna studio ambayo imeweza kupata bahati ya kuingiza bidhaa zake kwa wingi zaidi, yani nyimbo na wasanii pia. B'hits Music Studio kwa mwaka mwingine tena imeweza kuingiza bidhaa zake kwa wingi zaidi kuliko watayarishaji wengine. kwa mwaka uliopita B'hits iliingiza nyimbo nyingi zaidi na kufikia kuhusika na nyimbo za asili na nyimbo za Mduara kama "MTARIMBO", na mziki wa Reggae kwa wimbo wa "LEO(REGGAE VERSION)". 

Mwaka huu hali imekua hata nzuri zaid kwani wameweza kuhusika kama mara Kumi ukijumuisha na wasanii wake kama A.yPancho latino na Joh Makini kuwepo kwenye makundi ya machakato huo. Cha kuburudisha zaidi ni lile Kundi la Wimbo Bora wa Hip Hop ambao B'hits imeamua kuliteka na kulifanya la kwao. Hii inatokana na sababu ya kua na nyimbo tatu kati ya zile tano ndani ya kundi hilo..yani "usije mjini" ya Ay na MwanaFA, "karibu tena" ya Joh Makini na "Higher" ya Niki wa pili ambaye ni mdogo wake Joh Makini. Pia imeweza kutayarisha nyimbo mbili kati ya tano katika kundi la "wimbo bora afrika mashariki", na nyimbo hizo ni "songa mbele" ya Alpha na Ay na "Nitafanya" ya Kidum na Lady Jaydee, kitu ambacho ni mara ya kwanza kwani kundi hili kwa utamaduni ulozoeleka hutoa nyimbo zilizotayarishwa kutoka nje ya mipaka yetu. Na kwa mara nyingine tena imeweza kuingiza wimbo mwingine katika nyimbo za asili “Kariakoo” ya Mataluma na kama kawaida katika kundi la wimbo bora wa kushirikishwa kuna “Dakika Moja” ya Ay na MwanaFA bila kusahau nyimbo ya Linah “Bora Nikimbie” katika kundi la wimbo bora wa zouk/rhumba.

Hii ni faraja kubwa kwa B'hits na inaonyesha ukuaji ulio wazi wa ubora wa mziki na ubunifu wa sanaa ya mziki wa kizazi kipya. Hatuwezi kujua mwaka ujao utakua vipi lakini kwa hali halisi ambayo B'hits imeonyesha toka january mwaka huu hali inaonyesha itaku nzuri sanaa.

1.     AY B103-Msanii wa kiume bora wa muziki

2.     Pancho Latino R121-Mtayarishaji Bora wa Nyimbo

3.     Karibu tena -Joh Makini {Produced By Pancho Latino & Hermy B}J146-Wimbo Bora wa Hip Hop

4.     Usije Mjini -AY/Mwana FA{Produced By Pancho Latino & Hermy B} J182-Wimbo Bora wa Hip Hop

5.     Higher -Nick/Joh Makini {Produced By Pancho Latino & Hermy B}J142-Wimbo Bora wa Hip Hop

6.     Songa Mbele- Alpha/AY{Produced By Hermy B,Alpha & Elisha Butamu from Machozi Band} P176-Wimbo Bora wa Afrika Mashariki

7.     Nitafanya _Kidum/Jaydee{Produced By Hermy B & Kidum}P165-Wimbo Bora wa Afrika Mashariki

8.     Dakika moja -FA/AY/Hardmad{Produced By Hermy B & Pancho Latino} W137-Wimbo Bora wa Kushirikisha/Kushirikishwa

9.     Kariakoo -Mataluma {Produced By Pancho Latino}X145-Wimbo Bora wa Asili ya Kitanzania

10. Bora Nikimbie -Linah {Produced By Pancho Latino}Y135-Wimbo Bora wa Zouk/Rhumba

Hermes B. Joachim,
CEO B'Hits Music Group Tz,

            +255 713 513512       or             +255 785 513512     

No comments: