Ile amri ya serikali kuwataka wafanyabiashara kushusha bei ya sukari toka 2200 kwa kilo mpaka kufikia 1700 imezua mizengwe mingi nchini kwani viongozi wakati wanatoa kauli hii walitakiwa kufanya uchunguzi kwanza kwani mfuko wa sukari wa kg 25 unauzwa elfu 44 mpaka 45 kitu ambacho kinawashinda wanyabiashara wa rejareja kuuza sukari hiyo kwa 1700Tshs kwa kilo.
Hii inatokana ukweli kwamba wakati kauli hii inatoka wauzaji wa jumla walikuwa na stock kubwa ambayo waliinunua sukari hiyo kwa bei ya juu,kama serikali itaweza kuwafidia itakuwa makini zaidi ili sukari ishuke bei nchi nzima badala ya kustuka kuwa kiwanda kiko hapo na bei ya sukari inauzwa ghali kama sehemu ambazo hazina kiwanda karibu.
Habari kutoka kwa Unique Tz
No comments:
Post a Comment