Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mheshimiwa William Lukuvi
Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam Ofisini kwake kuhusiana na Tiba ya magonjwa sugu inayo tolewa na Babu Mchungaji Ambilikile Mwasapila huko Loliondo.Amesema kuwa serikari haina sababu ya kuzuia tiba hiyo kwa kuwa inahusisha imani za watu. "Serikali haina mpango wa kuzuia Huduma hiyo badala yake imeunda kamati itakayofanya kazi kwa kushirikiana na Mchungaji huyo ili kuhakikisha jamii inapata huduma hiyo kwa utaratibu unaostahili". Alisema lukuvi, alisema kamati hiyo inayo ongozwa na mkuu wa mkoa wa Arusha ambayo imeanza kazi jana, imezuia magari yote yanayokwenda kijijini hapo ili kutoa nafasi kwa Mchungaji Mwaisapila kuhudumia wagonjwa waliopo mpaka Idadi itakapo pungua.
Chanzo cha Habari:Jiachie Blog
No comments:
Post a Comment