Field Officer kutoka Shirika la Kihumbe, Salha Salim akitoa taarifa juu ya upokeaji na namna ya kutekeleza Mradi wa DREAM Kulia ni Mwandishi wa habari akisikiliza kwa makini. |
Baadhi ya Wajasiliamali wakiendelea na maandalizi ya kupanga bidhaa zao |
Watekelezaji wa Mradi wa DREAM wakiendelea na shughuli ya uelimishaji |
Wajasiliamali kutoka Shirika la Anglican wakiwa wamepanga bidhaa zao kwa ajili ya maonesho |
Muonekano wa Mabanda ya maonesho katika Uwanja wa Shule ya Msingi RuandaNzovwe jijini Mbeya. |
MAANDALIZI ya Sherehe za siku ya mtoto afrika sambamba na uzinduzi wa Mradi wa DREAMS
inatayofanyika kimkoa katika viwanja vya RuandaNzovwe jijini Mbeya Juni 16,
mwaka huu yamekamilika kwa asilimia kubwa..
Katika maadhimisho na Uzinduzi huo, Waziri Afya Jinsia,Wazee na watoto, Ummy Mwalimu anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi.
Mradi wa DREAM wenye lengo la kutoa elimu kwa wasichana kuanzia miaka 15 hadi 24 kuhusu
maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na Ukimwi utakaotekelezwa kwa miaka 2.
Akizungumzia maandalizi ya uzinduzi wa Mradi huo,
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Graciano Kunzugala alisema hadi sasa
washiriki wamefika eneo la tukio na kupanga bidhaa zao.
Alisema siku ya maadhimisho na Uzinduzi wa Mradi
wa DREAM unaofadhiliwa na Walter Reed Program(WRP) na kutekelezwa na Mashirika
ya Kihumbe na Anglican utakuwa na manufaa kwa watoto wa kike walio kwenye
hatari ya kupata maambukizi ya Virusi vya ukimwi.
Kunzugala alisema Hamasa kubwa imetolewa kwenye
mashirika ya Umma, Mashirika binafsi, Shule za Msingi hadi Vyuo vikuu ambapo
sherehe hizo zitapambwa na maonesho mbali mbali kutoka kwa wajasiliamali a Jiji
la Mbeya.
Aliongeza kuwa sambamba na maonesho ya
wajasiliamali pia Burudani zitatolewa ikiwemo Mpira wa Miguu utakaozihusisha
timu za Wasichana wenye Umri kati ya Miaka 15 hadi 24 kati ya Uyole na
RuandaNzovwe.
Alisema pia Elimu kuhusiana na afya na Ukimwi itatolewa, huduma za ushauri na upimaji pamoja
na Elimu ya Ujasiliamali itakayotolewa na Mashirika ya Kihumbe na Anglikan.
Alisema katika Sherehe hizo ambazo zitatanguliwa
na Maandamano makubwa yatakayoanzia Soweto hadi katika Viwanja vya RuandaNzovwe
ambako yatapokelewa na mgeni rasmi ambaye ni Waziri Ummy Mwalimu.
Kwa Upande wao Watekelezaji wa Mradi huo,
Shirika la Kihumbe walisema wameupokea vizuri Mradi wa DREAM na wajipanga
vizuri kuhakikisha wanautekeleza kama walivyopangiwa na muda muafaka.
Afisa wa Kihumbe, Salha Salim alisema maeneo
waliyopewa na kuyafanyia kazi ambayo tayari wameanza ni kuwatafuta na
kuwatambua walengwa wa Mradi ambao ni Wasichana waliokati ya miaka 15 hadi 24.
Aliwataja walengwa hao kuwa ni wasichana
waliokwenye hali hatarishi kama walioolewa kwenye umri mdogo, wanaokuwa wakuu
wa kaya na aliyefanyiwa ukatili wa kijinsia.
Aliongeza kuwa Shirika litawapatia watu hao
huduma zote zinazohitajika ndani ya Jiji la Mbeya ikiwa ni pamoja na Elimu ya
Ujasiliamali,elimu ya makuzi, Ushauri nasaha na upimaji wa hiari.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment