Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Bi. Mariam Mtunguja, akifungua
rasmi mkutano wa wadau wa PSPF uliofanyika Jijini Mbeya hivi
karibuni.
Afisa Mwandamizi wa PSPF, Bw. Msafiri Mugaka, akisoma hotuba
ya makaribisho kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu wakati wa mkutano wa wadau
wa PSPF uliofanyika Jijini Mbeya hivi karibuni.
Sehemu ya wadau waliohudhuria mkutano wa wadau wa PSPF
uliofanyika Jijini Mbeya
Afisa Mwandamizi wa PSPF, Bw. Msafiri Mugaka, akitoa elimu
kwa wadau wa PSPF katika mkutano uliofanyika Jijini Mbeya
Afisa Mfawidhi wa PSPF Mkoa wa Mbeya, Bw. Edwin Msavangwa,
akijibu hoja ya mmoja wa wadau katika mkutano wa wadau wa PSPF, kulia ni Afisa fedha Mwandamizi wa PSPF Bi. Hidaya Mganga.
Picha ya pamoja ya wajumbe wa mkutano wa wadau wa PSPF
pamoja na Mgeni Rasmi (katikati). Mkutano huo uliofanyika Jijini Mbeya hivi
karibuni.
Na Mwandishi wetu
PSPF
imesifiwa kwa kubuni bidhaa mpya kwa kuwanufaisha wanachama wake. Sifa hizo
zilitolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Bi. Mariam Mtunguja, alipokuwa
akifungua mkutano wa PSPF pamoja na wadau wake Mkoani Mbeya hivi karibuni.
Katibu
Tawala Mkoa Mbeya alisema kuwa mkopo wa elimu, mkopo kwa waajiriwa wapya na fao
la uzazi litakaloanza kutolewa Julai mwaka huu vitatoa haueni kwa wanachama wa
PSPF. “Kila mtu anaelewa jinsi vijana wetu wanavyopata tabu wanapoajiriwa,
kwani unapopata ajira au wakati wa uzazi mahitaji yanakuwa mengi sana, hivyo
kwa PSPF kuja na bidhaa hizi mpya mtakuwa mnasaidia vijana wetu kwa kiwango
kikubwa” alisema Bi. Mtunguja.
Kwa
upande wa mkopo wa elimu, Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, alipongeza PSPF kwa
kuunga mkono juhudi za Serikali za kuhakikisha kila mtanzania anapata elimu.
“Sisi wa upande wetu Serikalini tunajitahidi, lakini sasa tunafarijika kwa
kuona PSPF nanyi mnasaidia eneo hili muhimu, asanteni na hongereni.”
Katibu
Tawala Mkoa Mbeya aliishukuru PSPF kwa kutoa misaada katika maeneo elimu, afya,
uhifadhi wa mazingira na maendeleo ya jamii kwa lengo la kuunga mkono juhudi za
Serikali za kuhakikisha kila mtanzania anapata maisha bora.
Kwa
upande wa washiriki, Katibu Tawala Mkoa Mbeya, aliwaasa kutumia vizuri fursa
hii iliyotolewa na PSPF kwa kutatua changamoto wanazokabiliana nazo kuhusiana
na mafao ya wanachama wa PSPF na kupata ufafanuzi sahihi kutoka taarifa potofu
dhidi ya Mfuko.
Kwa
upande wa PSPF, mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Adam Mayingu , Bw.
Msafiri Mugaka, alisema Mfuko kwa upande wake umekuwa ukitekeleza vyema
miongozo na maelekezo kutoka Serikalini na mamlaka zote. Akiainisha changamoto
zilizopo, Bw. Mugaka, alisema changamoto kubwa ni kwa watumishi ambao
wanakaribia kustaafu kushindwa kuwasilisha nyaraka muhimu zinazohitajika hivyo
kuleta usumbufu kuandaa mafao kwa wakati. Aliomba wadau wa mkutano kuwaelimisha
wanachama wa PSPF juu ya umuhimu wa kuwa na nyaraka sahihi na kuziwasilisha kwa
wakati ili kuepusha usumbufu.
No comments:
Post a Comment