Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania (TAJATI) Ulimboka Mwakilili akitoa historia ya uanzishwaji wa Chama hicho kwa Watumishi wa Bandari ya Itungi. |
Watumishi wa Bandari pamoja na WanaTAJATI wakisikiliza kwa makini taarifa inayotolewa na Mkuu wa Bandari. |
ILI kuondokana na uharibifu wa
miundombinu ya barabara unaotokana na usafirishaji wa mizigo mizito kwa umbali
mrefu na kupelekea gharama kubwa kutumika katika ukarabati, Serikali imetakiwa
kuwekeza zaidi kwenye njia ya Maji na Reli.
Wito huo ulitolewa na Mkuu
wa Bandari ya Itungi iliyopo Kyela Mkoani Mbeya,Percival Salama, alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari kutoka Chama cha Waandishi wa habari za
Utalii na Uwekezaji Tanzania(TAJATI) waliofanya ziara bandarini hapo.
Salama alisema Serikali imekuwa
ikitumia gharama kubwa kukarabati na kutengeneza miundombinu ya barabara ambayo
huharibika kutokana na usafirishaji wa mizigo mizito jambo ambalo huingizia
hasara taifa.
Alisema ili kukabiliana na
changamoto ya miundombinu ya barabara ni vema Serikali ikajikita katika
kuboresha miundombinu ya Reli na usafiri wa majini kwa kuwa ndiyo unaweza
kusafirisha mizigo mikubwa zaidi bila kuharibu miundombinu.
Alisema pia usafiri wa Reli na
Maji ni rahisi hata kwa mfanyabiashara anayesafirisha biashara zake kutokana na
mzunguko wake kuwa mfupi tofauti na matumizi ya barabara ambazo mara nyingi
umbali wake ni mrefu.
Meneja huyo alitolea Mfano
usafirishaji wa makaa yam awe kutoka Mbinga mkoani Ruvuma hadi Kiwanda cha
Saruji cha Mbeya kilichopo Songwe kuwa husafiri kwa Kilomita 520 lakini endapo
wangesafirishia Meli wangekuwa wanasafiri kilomita 420 tu hivyo kuokoa hata
muda.
“Serikali ingetakiwa kujenga
Reli kutoka Uyole hadi Kyela Itungi Port ambayo urefu wake hauzidi Kilomita 100
ambapo mizigo mingi inaweza kusafirishwa hadi ziwani kasha huingia kwenye meli
hivyo kuondoa uharibifu wa miundombinu ya barabara na gharama kuwa nafuu”
alisema Salama.
Aliongeza kuwa ujenzi wa Reli kutoka Uyole jijini Mbeya
hadi bandari ya Itungi Kyela ukiunganishwa na Reli ya Tazara utasaidia
kurahisisha usafirishaji wa mizigo mikubwa kupitia Meli na Reli baada ya
kukamilika kwa Meli kubwa za Mizigo zinazojengwa katika Bandari ya Itungi.
Alisema Meli zinazojengwa hapo
zinatarajia kukamilika mwezi Agosti na Oktoba mwaka huu ambazo zitakuwa na
uwezo wa kubeba na kusafirisha mizigo ya Tani 566.166 kila moja kwa wakati
mmoja.
Aliongeza kuwa ilikuwa ni vema
baada ya mizigo kushushwa katika bandari ya Itungi kutoka upande mwingine wa
Ziwa ikabebwa kwa Reli na kuwapelekea wahusika na sio kusafirisha kwa barabara
ili kutoziharibu kwa matumizi mengine.
Meneja Salama alisema
kukamilika kwa ujenzi wa Meli hizo zinazojengwa na Mkandarasi mzawa kutoka
Kampuni ya Songolo Marine transport Botyard
utatoa fursa kwa makampuni kusafirisha bidhaa zao pamoja na malighafi kiurahisi.
Alisema hivi sasa kuna upungufu
mkubwa wa usafirishaji wa mizigo katika bandari ya Itungi hali iliyotokana na
kuharibika kwa Meli na kwamba mwaka 2011/2012 makaa yam awe pekee
yalisafirishwa tani 26000 huku matarajio yakiwa ni tani 66000.
No comments:
Post a Comment