Meneja wa Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe uliopo mkoani Mbeya, Hamis Amir akifafanua jambo kwa Waandishi wa habari kutoka TAJATI (hawapo pichani). |
Meneja wa Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe uliopo mkoani Mbeya, Hamis Amir akifafanua jambo kwa Waandishi wa habari kutoka TAJATI. |
Meneja wa Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe uliopo mkoani Mbeya, Hamis Amir akiwatembeza Waandishi wa habari kutoka TAJATI. |
Meneja wa Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe uliopo mkoani Mbeya, Hamis Amir akifafanua jambo kwa Waandishi wa habari kutoka TAJATI |
Jengo la abiria ambalo halijakamilika. |
Meneja wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Kanda, Issa Hamad akitoa maelezo kwa Wana TAJATI. |
Muonekano wa majengo katika uwanja wa ndege Songwe |
Muonekano wa Uwanja wa ndege wa Songwe. |
Senior Breafing officer wa Songwe airport akifafanua jambo |
Muongoza ndege Bertila Ngowi akitoa maelezo na changamoto zinazowakabili. |
ILI
kuongeza idadi ya Wawekezaji na Watalii kwa Mikoa ya Nyanda za Juu kusini,
Serikali imetakiwa kukamilisha mara moja ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa kimataifa
wa Songwe uliopo mkoani hapa.
Imeelezwa
kuwa ikiwa uwanja huo ukimaliziwa idadi kubwa ya Watalii na ndege kubwa
zitaweza kutua na kuongeza wawekezaji na kutoa fursa za kiuchumi kwa
wakazi wa mikoa ya nyanda za juu.
Wito
huo ulitolewa na Kaimu Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe, Hamisi
Amiri,alipokuwa akizungumza na Wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari za
Utalii na Uwekezaji nchini(TAJATI)katika mwendelezo wa ziara zake nchini kuibua
fursa za utalii na uwekezaji.
Amiri
alisema hivi sasa uwanja huo unakabiliwa na Changamoto ya Jengo la kufikia
abiria ambalo ujenzi wake umekwama kwa muda wa mwaka mmoja sasa kutokana na
ukosefu wa fedha.
“jengo
la kufikia abiria limekwama kuendelea na ujenzi kwa zaidi ya mwaka mmoja hivi
sasa kutokana na serikali kukosa fedha za kumlipa mkandarasi zaidi ya shilingi
bilioni kumi na moja kazi ambayo ingemalizika kwa kipindi cha miezi sita kama
pesa zingekuwepo”alisema Meneja huyo.
Alisema
Serikali imetoa pesa kwa ajili ya ufungwaji wa taa katika njia ya kurukia ndege
hivyo kuondoa adha ambayo wanakumbana nayo marubani wakati wa kutua na kuruka
pindi kunapotokea hali ya mawingu katika uwanja huo ambao upo kwenye ukanda wa
bonde la ufa.
Kwa
upande wake Afisa usafirishaji wa abiria katika uwanja huo Jordan Mchami
alisema kukamilika kwa jengo la abiria kutasaidia kuongezeka kwa mashirika
mengine ya ndege ya kimataifa na kuongezeka kwa abiria na kwamba jengo hilo
linaweza kupokea abiria zaidi ya elfu moja kwa wakati mmoja.
Baadhi
ya waongozaji wa Ndege katika uwanja huo walisema changamoto kubwa inayo
wakabili katika uwanja huo ni pamoja na marubani kukumbana na hali ya
ukungu na ukosefu wa taa katika barabara ya kurukia ndege ambapo mara kadhaa
ndege zimekuwa zikishindwa kutua kwa wakati na pengine kurudi zilikotoka
kutokana na hali hiyo.
Katika
hitimisho la ziara hiyo Meneja wa Uwanja wa Ndege Amiri Hamisi alisema
waandishi wa Habari wana nafasi kubwa katika mchango wa uchumi kama
ambavyo wameweza kuokoa uwanja mdogo wa zamani uliopo Kata ya Iyela uliokuwa
umevamiwa na baadhi ya viwanja kuuzwa na baadhi ya wananchi kwa kushirikiana na
mamlaka za umma.
Amiri
alisema Waandishi baada ya kuitoa habari hiyo Serikali imetoa shilingi milioni
mia sita(600,000/=) kwa ajili ya upimaji na umiliki kisheria ili kuzuia uvamizi
ikiwa ni pamoja na kuweka uzio kwa ajili ya usalama ili kuzuia mifugo na watu
wanaokatiza uwanjani pindi ndege zinapotua na kuruka katika uwanja wa ndege wa
Songwe.
Ziara
hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Ulimboka Mwakilili ilitembelea
huduma mbalimbali katika uwanja huo kama Idara ya Utabiri wa Hali ya
Hewa,Kikosi cha Zimamoto na uokoaji,Uongozaji wa Ndege na Huduma za
usafirishaji wa abiria.
Kwa
upande wake Meneja wa Mamlaka wa Hali ya Hewa,Kanya ya Nyanda za juu kusini,
Issah Hamadi alisema Idara hiyo ina vituo mbalimbali vya utabiri wa hali ya
hewa ambavyo husaidia katika shughuli za anga na Kilimo na kwamba kituo hicho
kilianzishwa mwaka 1929.
Issah
alisema kituo hicho ambacho hufanya shughuli zake uwanja wa ndege wa zamani na
Songwe kimepata tuzo ulimwenguni kutokana na huduma bora za utabiri wa hali ya
hewa hivyo kuleta heshima kwa Taifa kutokana na utendaji wake bora.