|
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Nyerembe Munasa Sabi akitoa hotuba katika uzinduzi wa ofisi za Kampuni ya Umeme jua ya OFFGRID ELECTRIC maarufu kwa jina la Mpower. |
|
Meneja Operesheni Kanda ya Kati na Kusini wa Mpower, Emmanuel Ng'andu akitoa taarifa ya mradi wa Mpower wakati wa hafla ya kuzindua Ofisi za Kampuni hiyo mkoani Mbeya. |
|
Meneja wa Mpower Mkoa wa Mbeya, Godlisten Shayo akitambulisha baadhi ya watumishi wa Kampuni hiyo pamoja na idadi ya wateja walionufaika na miradi ya Mpower. |
|
Diwani wa Kata ya Ilomba akitoa taarifa kuhusu jinsi wananchi walivyoupokea Mradi wa Mpower na kuukubali |
|
Mmoja wa Wateja walionufaika na huduma za Mpower akitoa ushuhuda wake |
|
Mmoja wa Wateja walionufaika na huduma za Mpower akitoa ushuhuda wake |
|
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyerembe Munasa akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ofisi ya Mpower Veta jijini Mbeya. |
|
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyerembe Munasa akipata maelezo juu ya mitambo ya Mpower baada ya kuzindua ofisi. |
|
Meneja masoko wa Mpower Mkoa wa Mbeya, Kaluse Kiangi akitoa maelezo kwa wageni mbali mbali kuhusiana na huduma zinazotolewa na Mpower |
|
Picha ya pamoja ya baadhi ya watumishi wa Mpower, Wateja na wageni waalikwa |
|
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya akigonganisha grasi na Meneja Oparesheni baada ya kuzindua ofisi ya Mpower Mkoa wa Mbeya |
|
Mfanyakazi wa Mpower akifungua shampeni |
|
Kiongozi wa Mila wa Kata ya Ilomba akimiminiwa kinywaji |
|
Meneja wa Mpower Mkoa wa Mbeya akikata keki kwa ajili ya sherehe ya uzinduzi wa ofisi |
|
Baadhi ya Wananchi na Wateja wa huduma za Mpower wakifuatilia kwa makini sherehe za uzinduzi wa Ofisi Mkoa wa Mbeya. |
KAMPUNI ya Umeme jua ya OFFGRID
ELECTRIC maarufu kwa jina la Mpower imezindua Tawi lake Mkoani Mbeya ambapo
tayari Wakazi wa Jiji la Mbeya wameanza kunufaika.
Akitoa taarifa kwa Mkuu wa
Wilaya wakati wa uzinduzi wa Ofisi hizo zilizopo eneo la Veta kata ya Ilomba,
Oparesheni Meneja wa Offgrid Elictric(Mpower)Kanda ya Kati na Kusini, Emmanuel
Ng’andu alisema mradi wa Mpower ulianza 2012 ukiwa na lengo la kuwafikia
wananchi ambao hawana umeme wa grid ya taifa.
Ng’andu alisema Mradi huo
unatekelezwa katika Nchi mbili barani Afrika ambazo ni Tanzania na Rwanda na
kwamba kwa nchini Tanzania tayari mikoa 15 imefikiwa ukiwemo Mkoa wa Mbeya.
Alisema tangu mradi umeanza
kaya 120,000 kwa wastani wa kila kaya kuwa na watu watano hivyo takribani watu
600,000 wamefikiwa na kuanza kutumia huduma za Mpower nchini na kusaidia
upatikanaji wa maendeleo.
Aliongeza kuwa Mradi huo
umeingia Mkoa wa Mbeya mwanzoni mwa mwezi Mei na kuanza kutekelezwa katika Kata
za Ilemi, Itezi na Ilomba ambapo tayari Kaya 100 sawa na watu 500 wamenufaika.
Alisema mbali na kuwafikia
wananchi pia katika mikoa ambayo mradi huo umepita pia wanatoa msaada katika
huduma za jamii kwa kuingiza umeme wa jua katika Vituo vya afya, Shule za bweni
na vituo vya Polisi.
Meneja huyo alisema Kampuni
hiyo inayo mtambo wa kujua mteja alipo kwa njia ya majira ya nukta(GPS), mfumo
wa malipo kwa njia ya simu za mkononi ili kumrahisishia mteja kupata huduma
kirahisi pamoja na kutoa huduma kwa wateja bila gharama yoyote na bila kujali
sehemu alipo.
Kwa upande wake Mgeni rasmi
katika uzinduzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya alipongeza ujio wa Kampuni hiyo na
kwamba itakuwa kichocheo cha maendeleo kwa Mkoa wa Mbeya.
Munasa alisema uwepo wa kampuni
hiyo ya Mpower ni mapinduzi makubwa ya kimaendeleo ambayo yamekuja katika
kipindi ambacho Jiji la Mbeya linajipanga ili liweze kuwa Stahimilivu na kuweza
kujiendesha pasipokuwepo kwa Nishati za aina zozote kama ilivyo kwa Majiji
mengine ya Ulaya.
Aliongeza kuwa uwepo wa Kampuni
ya Mpower kutawanufaisha wakazi wengi wa Jiji la Mbeya katika kipindi hiki
ambacho zaidi ya asilimia 80 wananchi wako kwenye makazi yasiyorasmi hivyo njia
pekee ni kupata umeme wa Jua.
2 comments:
Na pia kwa wateja wote ambao wangependa kujua zaidi huduma za Solar za M-Power tafdhali wasiliana nasi bure kwa namba 0800752222
Na pia kwa wateja wote ambao wangependa kujua zaidi huduma za Solar za M-Power tafdhali wasiliana nasi bure kwa namba 0800752222
Post a Comment