Katika miaka ya hivi
karibuni ufugaji wa kuku umekua kwa kiasi kikubwa na kuwa mtaji mkuu wa
wajasiriamali wadogo na wakubwa katika kujiingizia kipato.
Hata hivyo ufugaji wa
kuku nao umekuwa ukienda kwa wakati kutokana na ukuaji wa teknolojia. Moja ya
teknolojia hizo ni mashine za kutotoleshea vifaranga kitaalamu; ‘incubator’.
Mary David maarufu kama
‘Mama Kuku’ ni Mkurugenzi wa Kuku Project Tanzania, ambaye pia ni msambazaji wa
mashine za kisasa za Incubator, yeye anasema kuwa mashine hizo zimekuwa
mkombozi kwa wafugaji wa kuku nchini kwa kuwa huuzwa kwa bei rahisi inayoendana
na mahitaji ya mfugaji mwenyewe.
“Incubator zetu ni za
bei tofauti kuanzia shilingi laki nne na nusu ambazo zina uwezo wa kubeba mayai
arobaini na nane na kubwa kabisa ambayo hubeba mayai elfu kumi na tisa mia saba
kumi na mbili ambayo huuzwa kwa shilingi milioni ishirini,” anasema Bi. Mary.
Mbali na hayo, Bi. Mary
anasema kuwa incubator hizo huwa na uwezo wa kutumia umeme, nishati ya jua na
pia kuhifadhi umeme kwa masaa sita baada ya umeme kukatika ambapo pia mtumiaji atapata fursa ya
kuelekezwa jinsi ya utumiaji wake huku mashine hizo zikiwa na waranti ya mwaka
mzima.
Kwa maelezo zaidi na
jinsi ya kununua Incubator fika DAR ES SALAAM,MAGOMENI MWEMBE CHAI,NYUMA YA
KANISA LA WASABATO. SIMU : +255 653 691
138+255 715 908 307,+255 678 226 988
Kujua zaidi Like Page yao kwa kubofya hapa chini :
No comments:
Post a Comment