Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari |
Baadhi ya Wafanyabiashara wakilalamikia Chumba kilichokuwa kimetengwa kwa ajili ya Dampo kudaiwa kupangishwa kwa Mfanyabiashara kinyume na matumizi yaliyokusudiwa |
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya wakipita mbele ya Vizimba vya wafanyabiashara wadogo ambavyo pia havitumiki kutokana na kodi kuwa kubwa |
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akikagua Soko la Mwanjelwa |
MKUU wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla amewaagiza Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kwa kuisimamia Halmashauri ili isonge mbele katika shughuli za maendeleo.
Agizo hilo alilitoa katika
ziara yake ya kujitambulisha alipokuwa akiongeza na madiwani, watumishi wa
halmashauri, viongozi wa mila na viongozi wa dini katika mkutano uliofanyika
kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.
Makalla alisema Madiwani
wanayonafasi ya kuisimamia Halmashauri kwa kuhakikisha miradi yote inatekelezwa
kama inavyotakiwa, pamoja na kusimamia asilimia kumi za mapato kwenda kwenye
mikopo ya vikundi vya Vijana na akina
mama.
“Kazi ya madiwani sio kususia
vikao na kudai posho, nyie majukumu yenu ni kuisimamia halmashauri kwa kuhakikisha
miradi inatekelezwa na zile asilimia kumi zinatengwa na kuwafikia walengwa,
kwanza itakuongezea kura kwenye uchaguzi ujao” alisema Mkuu wa Mkoa.
Makalla alisema Madiwani
hawapaswi kupokea posho za vikao kama kikao kitakuwa kimevunjika lengo likiwa
ni kubana matumizi na kuokoa fedha kwa ajili ya shughuli za maendeleo.
Aidha aliwanyoshea vidole
Watendaji wa Kata na vijiji pamoja na viongozi wote kuanzia ngazi ya kijiji
kuhakikisha wanasoma mapato na matumizi kwa wananchi ya fedha walizochangia.
“Wasiosoma mapato na matumizi
siku zao zinahesabika, haiwezekani mradi mmoja haujakamilika mnawachangisha
wananchi michango mingine hapo lazima kuna ufisadi ambao mbele yake utasababisha migogoro katika jamii”
alisisitiza Makalla.
Mkuu huyo wa Mkoa aliagiza kuwa
mwaka wa fedha 2016/2017 ni marufuku mawakala kutumika kukusanya ushuru ndani
ya halmashauri bali kazi hiyo inapaswa kufanywa na watumishi wenyewe.
“Ni marufuku mawakala kutumika
kukusanya mapato kwanzia mwaka wa fedha ujao kwani wanasababisha kero kwa
wananchi pia wao wanapata faida kubwa kuliko halmashauri, watumishi wako wengi
wengine wanakaa maofisini bure tu hivyo watakaa kwenye mageti kukusanya ushuru
kwa kutumia mashine ya kielekroniki” aliagiza Makalla.
Wakati huo huo Makalla aliagiza
Watumishi wote katika Mkoa wa Mbeya kurudi kwenye vituo vyao vya kazi kwa ajili
ya kuhakikiwa upya ambapo alitoa kuanzia tarehe 20 hadi 24 Aprili 2016 kuwa
muda wa kusafiri na kwamba zoezi litaanza Aprili 25 hadi 29,mwaka huu.
Alisema amelazimika kurudia
zoezi la kuhakiki baada ya kubainika kuongezeka kwa watumishi hewa katika
Halmashauri ya Jiji na Wilaya ya Mbeya ambapo Halmashauri ya Wilaya imeongezeka
kutoka watumishi 9 hadi 13 huku Jiji wakiongezeka kutoka 14 hadi 23.
Alisema ili kufanikisha zoezi
hilo ameunda kikosi cha watu 14 ambapo mtumishi atapaswa kuonekana kwa sura
akiwa na barua ya kazi, kitambulisho na slipu ya Mshahara wa mwisho wa mwezi.
No comments:
Post a Comment