Muonekano wa Ofisi za Uwanja wa ndege wa Zamani wa Mbeya unaodaiwa kuvamiwa |
Mwenyekiti wa Mtaa wa Airport, Enock Mwampagama akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu uvamizi wa Uwanja wa ndege |
Baadhi ya Waandishi wa habari wakipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Airport |
Baadhi ya Waandishi wakiangalia mawe (bikons) zilizowekwa katika mashamba ambayo wananchi wamepimiwa ndani ya Uwanja wa Ndege |
Moja ya Jiwe likionesha kiwanja kilichopimwa |
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Pambogo wakicheza kwenye uwanja wa Ndege ambapo wanalia kukosa eneo la kuchezea licha ya watu kugawana maeneo |
Njia ya kurukia ndege ambayo sasa imegeuka uwanja wa kujifunzia kuendeshea magari |
MUDA mfupi kupita baada ya Serikali
kujenga na kuzindua Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Songwe uliopo Wilaya ya
Mbeya Mkoani Hapa, Baadhi ya Wananchi wameanza kujipimia na kugawana uliokuwa
Uwanja wa ndege wa zamani uliopo Iyela jijini Mbeya kwa matumizi binafsi.
Idadi ya viwanja vinavyodaiwa
kuuzwa ni kati ya 60 hadi 70 ambapo jopo la wanahabari wa Chama Cha Waandishi
wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania (TAJATI) walitembelea na kukuta mawe
yaliyopimwa kwa ajili ya kuwagawia wananchi.
Imeelezwa kuwa viwanja hivyo vyenye
thamani ya kuanzia sh mil 20 hadi sh mil 50 kila kimoja vimegawiwa kwa wananchi
huku ikielezwa kuwa mmoja wa wakazi wa eneo hilo aliyefahamika kwa jina la
Mwanguku kuwa ndiye anayemiliki eneo hilo kabla ya kuanzishwa kwa uwanja huo
zaidi ya miaka 50 iliyopita.
Uwanja huo wenye urefu unaokadiriwa
km 2.7 uliopo Iyela jijini Mbeya umedaiwa kuuzwa kwa wananchi wa eneo hilo huku
kukiwa na madai kuwa baadhi ya Watumishi wa Halmsahauri ya Jiji la Mbeya wanahusika
na uuzwaji wa eneo la uwanja huo.
Akizungumza na waandishi wa habari
kutoka TAJATI, Mwenyekiti wa Mtaa wa Airport, Enock Mwampagama alikiri kuona
uwanja huo umevamiwa huku kukiwa na baadhi ya viwanja vilivyopimwa na baadhi ya
watu wakiendelea kulima eneo hilo.
Naye Mwenyekiti wa mtaa wa Pambogo
ambako uwanja huo umepakana na mtaa huo Esia Edward, alisema mara baada ya kuona eneo hilo linavamiwa
alitoa taarifa ya uvamizi huo serikalini ambako hakupata mrejesho juu ya
uvamizi huo.
Mwenyekiti wa mtaa wa Block T
Adrian Majembe, alisema ameona uvamizi
mkubwa ukiendelea eneo hilo na kuwa hata hivyo yeye kama Mwenyekiti wa mtaa
unaopakana na uwanja huo hakushirikishwa kwa lolote na kuwa amesikia eneo hilo
la viwanja lilikuwa ni la familia ya mtu aliyetambulika kwa jina la Mwanguku
ambaye inadaiwa eneo hilo ni mali ya familia hiyo.
Alisema wakazi wa eneo hilo walidai
kuwa eneo hilo wamegaiwa na Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi
alipokuja Jijini Mbeya.
Alisema hata yeye alisikia watu
wakisema wananchi wamegawiwa viwanja na wameruhusiwa kujenga eneo hilo na
Waziri Lukuvi, Majembe ambaye aliwahi kuwa Meya wa Manispaa ya Mbeya kati
ya mwaka 1994-2000.
Kwa upande wake Ofisa Mtendaji wa
Kata ya Iyela Henry Shipela alisema mara alipopata taarifa za uvamizi wa eneo
hilo alifuatilia na kukuta watu wakiwa wanalima na kuwa baada ya kuulizia
baadhi ya watu akaambiwa kuwa ni familia ya watumishi wa uwanja wa ndege na
kuwa hata hivyo atafuatilia kujua sababu zaidi juu ya uvamizi wa uwanja huo.
Akizungumzia suala la uvamizi wa
uwanja huo Meneja wa Uwanja wa Kimataifa wa Songwe, Hamis Amir, alisema amesikia suala la uvamizi wa uwanja ndege wa
Iyela ambao ulikuwa ukitumika awali kabla ya kuanzishwa kwa uwanja wa Songwe
mwaka 2012 lakini hata hivyo hajui vyema mipaka ya uwanja huo.
Mmoja wa maofisa wa Halmashauri ya
Jiji anayeelezwa alihusika katika upimaji huo aliyetambulika kwa jina la Ben
Mponzi alisema kuwa uwanja huo ulipimwa na Ofisa Mpima Ardhi wa Jiji la Mbeya
Athuman Maugo ambaye naye alidai kuwa eneo hilo lilipimwa kwa idhini ya
serikali na si Halmashauri ya Jiji la Mbeya.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la
Mbeya Dkt Samwel Lazaro, alisema Halmashauri ya Jiji la Mbeya haihusiki na
jambo lolote kuhusu uwanja wa ndege wa Airport.
Awali Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya,
Mariam Mtunguja alisema Serikali ya Mkoa imeandika barua serikali kuu ili
kuomba kibali cha kubadili matumizi ya uwanja huo ikiwa ni kutumia katika sekta
ya uwekezaji.
No comments:
Post a Comment