Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, February 15, 2016

VIJANA WATAKIWA KUTUMIA MCHEZO WA MPIRA KAMA AJIRA

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Nerembe Muanasa akifundisha namna mchezaji wa mpira wa miguu anavyoweza kufunga mpira kisayansi alipokuwa akifundisha katika Kliniki ya michezo iliyofanyika katika uwanja wa Sokoine.

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Nyerembe Munasa akitoa maelekezo kwa wachezaji wakati wa kliniki ya Michezo iliyofanyika uwanja wa Sokoine jijini

Wachezaji waliohudhuria kliniki ya michezo wakijadiliana moja ya somo

Wachezaji wakifuatilia somo la michezo

Wachezaji wakiwa katika mazoezi ya vitendo katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya
 
VIJANA wametakiwa kucheza mpira kama ajira ili kufikia malengo ya kucheza kombe la dunia na hatimaye kupata nafasi ya kucheza soka la kulipwa.
 
Wito huo ulitolewa  na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Nyerembe Munasa alipokuwa akitoa mafunzo ya Ulinzi na Ushambuliaji kwa vijana yanayofanyika katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
 
Mafunzo ya siku tatu ya kliniki ya michezo kwa ajili ya ulinzi na ushambuliaji yalifunguliwa na Mdau wa Michezo nchini Ndele  Mwaselela katika Uwanja wa Sokoine Jijijini Mbeya yatakayodumu kwa siku tatu kuanzia Februari 12 hadi 14 mwaka huu.
 
Akifungua mafunzo hayo,Mwaselela aliwataka vijana kushiriki kikamilifu mafunzo hayo ili yaweze pia kuwapatia ajira.
 
Ndele alisema kuwa Washiriki wakizingatia mafunzo hayo ambayo ni adimu nchini yatawawezesha kwenda nje ya nchi ili kupata mafunzo katika shule rafiki iliyopo Ujerumani.
 
Akifungua mafunzo hayo Mgeni rasmi ametoa shilingi laki nane ili kufanikisha mafunzo hayo yanayogharimu zaidi ya shilingi milioni moja kwa ajili ya chakula na vifaa vya kufundishia.
 
Kwa upande wake Mkufunzi wa mafunzo hayo Nyerembe Munasa alisema kuwa mafunzo hayo ya siku tatu  yatawajengea uwezo  wa mbinu stadi na ufundi ambao baadhi yao wamenufaika kwa kwenda nje ya nchi kama Afrka Kusini na Brazil kwa mafunzo zaidi.
 
Munasa ambaye ni Mmililiki wa Kituo cha Elimu Mwendo(Human Kinetics Academy)alisema atatoa mafunzo hayo ya siku tatu kwa vijana zaidi ya mia moja Jijini Mbeya  wakizingatia vipaji vya Soka nchini na kuweza kutoa wachezaji wa kimataifa.
 
Mmoja wa Washiriki wa mafunzo hayo kutoka kituo cha Elimu Mwendo kwa niaba ya washiriki amemshukuru Mwezeshaji wa mafunzo hayo na Mgeni rasmi kwa kupata mafunzo hayo ambayo yatawasidia katika soka.
 
Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya Harub Seleman amempongeza Mkufunzi wa semina hiyo na kumuomba asikatishwe tamaa kwa mahudhurio hafifu ya washiriki na kwamba waliotarajiwa kushiriki mafunzo ni zaidi ya 200 lakini waliohudhuria si zaidi ya 30.
 
Mafunzo hayo yatamalizika Februari 14 katika Uwanja wa Sokoine na kuwawezesha kumudu ulinzi na ushambuliaji kisayansi hivyo kulifanya soka la Tanzania kuwa la kisasa.
 

No comments: