Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, November 23, 2015

JIJI LA MBEYA LAANZISHA IDARA YA HABARI KURAHISISHA MAWASILIANO.


Mkuu wa Idara ya Utawala na Utumishi Jiji la Mbeya akizungumza na waandishi wa Habari kwa niaba ya Mkurugenzi.


Maafisa Habari wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Jacqueline Msuya na John Kilua wakifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari wakati wakijitambulisha.

Afisa habari wa Jiji la Mbeya, John Kilua akiomba ushirikiano kwa waandishi wa habari Mbeya.


Baadhi ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya wakiwa katika mahojiano na maafisa Habari wa Jiji la Mbeya katika Mkutano wa kutambulishwa.


OFISI ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya Mkoani hapa imeajiri maafisa Habari ili kurahisisha mawasiliano baina ya Mkurugenzi, Wananchi na waandishi wa habari.

Akizungumza na waandishi wa habari wa habari wakati wa utambulisho wa Maafisa hao, Mkuu wa Idara ya Utawala na Utumishi Halmashauri ya Jiji la Mbeya.Erick Mapunda kwa niaba ya Mkurugenzi alisema lengo ni kuwa daraja kati ya wananchi na waandishi wa habari katika kuboresha utumishi wa umma.

Aliwatambulisha maafisa hao kuwa ni Jacqueline Msuya na John Kilua ambao alisema mbali na kuwa daraja baina ya waandishi na Ofisi ya Mkurugenzi pia itasaidia kuboresha mahusiano kati ya watumishi wa Halmashauri na waandishi wa habari.

Kwa upande wao Maafisa hao walisema kutokana na kuwepo kwa kitengo hicho Waandishi wa habari watapaswa kufuata utaratibu endapo watakuwa na shida ya kupata ufafanuzi kutoka kwa Mkurugenzi au mkuu wa idara.

Walisema ni vema Mwandishi wa habari akapata kibali kutoka kwa Afisa habari ya kwenda kuonana na mhusika endapo suala lake litakosa majibu kutoka katika ofisi ya Idara ya Habari ili kuondoa usumbufu wa kurudishwa na kukosa ushirikiano.

No comments: