Balozi
wa Imetosha,Henry Mdimu (kati) azungumza na waandishi wa habari (hawapo
pichani) wakati azungumzia harakati zake za kutaka kwenda kanda ya Ziwa
ili kuihamasisha jamii juu ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa
ngozi.Kulia ni Mwenyekiti wa Imetosha Movment,Masoud Ali "Kipanya" na
kushoto ni Monica Joseph mjumbe wa Imetosha.
Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network ambao ni Wajumbe wa Imetosha,Joachim Mushi akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo.
Baadhi ya Wajumbe wa Imetosha wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Na Chalila Kibuda
Balozi
wa Imetosha,Henry Mdimu amewataka watu wajitokeze katika harakati za
kupambana na watu wenye imani potofu za kuwaua watu wenye ulemavu wa
ngozi (Albino).
Mdimu
amesema uchunguzi umebaini ukosefu wa elimu kwa watu wenye imani hizo
ndiyo hupelekea mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi hivyo silaha ya
elimu ni sehemu kubwa ya harakati hapa nchini.
Hayo
ameyasema leo wakati alipokutana na waandishi wa habari jijini Dar es
salaam na kusema kuwa ana mpango wa kwenda kanda ya Ziwa ili
kuihamasisha jamii juu ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi.
Aidha,Mdimu
ameahidi kutoa elimu hiyo kwa njia ya sanaa kwa kuwatumia baadhi ya
wasanii kama Jhikoman,Kassim Mganga,Profesa J,Ray C,Fid Q,Roma Mkatoliki
pamoja na Dami Msimamo.
Pia
amevitaka Vyombo vya Habari kutoa ushirikiano katika harakati hizo za
kuhakikisha wanatokomeza mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi.
Na Michuzi Blog
Na Michuzi Blog
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
No comments:
Post a Comment