Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro
akitoa hotuba wakati akifungua semina kwa ajili ya Maafisa Rasilimali watu Mkoa
wa Mbeya iliyoandaliwa na mfuko wa hifadhi ya jamii wa GEPF.
|
Meneja Biashara wa GEPF Taifa,
Aloyce Ntukamazina akitoa taarifa ya mfuko la lengo la Semina kwa washiriki wa
semina hiyo.
|
Meneja
Biashara wa GEPF Taifa, Aloyce Ntukamazina akitoa mada katika semina kwa
Maafisa Rasilimali watu Mkoa wa Mbeya.
|
Washiriki
wa semina wakisikiliza mada zinazowasilishwa kuhusiana na mfuko wa GEPF.
|
Washiriki
wa Semina wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.
|
MKUU
wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, amewataka wananchi wote kujenga utamaduni wa
kujiunga na mifuko ya hifadhi za jamii kwa ajili ya manufaa ya uzeeni na
kupunguza malalamiko.
Kandoro
alitoa wito huo alipokuwa akifungua semina kwa ajili ya Maafisa
rasilimali watu wa Mkoa wa Mbeya iliyoandaliwa na Mfuko wa pensheni wa GEPF,
iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Hill view Uzunguni jijini hapa.
Alisema
kuna dhana iliyojengeka miongoni mwa jamii kuhusu mifuko ya hifadhi za jamii
kuwa ipo kwa ajili ya waajiriwa wa serikali tu jambo ambalo ni kinyume kwani
kila Mtu ana haki ya kujiunga na mfuko wowote anaoutaka kwa ajili ya manufaa ya
baadaye.
Alisema
mifuko hiyo ipo kwa ajili ya uwekaji wa akiba kwa hiari kwa mwajiriwa wa
serikali na aliyejiajiri mwenyewe kama Mkulima, Mfanyabiashara,mfugaji,
machinga, madereva wa bodaboda, bajaji na wajasiliamali wadogo ambao kwa mujibu
wa sera wanapaswa kujiunga bure.
Aidha
alitoa wito kwa wenye mifuko kuhakikisha inaendesha mambo yake kwa uwazi na
kuimarisha mfumo wa Tehama ili utoaji taarifa kwa wanachama uwe sahihi na kwa
wakati wote.
Aliongeza
kuwa mifuko hususani GEPF iwe na utaratibu wa kuwafuatilia wanachama wake
kuhakikisha michango inafika kwa wakati na sio kukaa maofisini kusubiria
mwajiri kupeleka ili hali kuna wengine hawapeleki makato ya waajiriwa wao jambo
ambalo litasaidia kuondoa migogoro isiyokuwa ya lazima.
Awali
akimkaribisha Mkuu wa Mkoa, Meneja Masoko wa GEPF taifa,Aloyce Ntukamazina,
alisema sababu ya kuendesha semina hiyo kwa Maafisa rasilimali watu wa Mkoa wa
Mbeya ni kutokana na wao kuwa ndiyo washauri na waajiri wa watumishi wageni.
Aliongeza
kuwa sababu nyingine ni kuza Mfuko huo Mbeya, mabadiliko makubwa ya mifuko
nchini hivyo kuwa na umuhimu wa kutoa semina elekezi kwa wadau ambao ndiyo
waajiri wakubwa.
Alisema
pia kuna mabadiliko makubwa ya kimfumo katika mfuko wa GEPF pamoja na ongezeko
la mafao ambapo pia Afisa rasilimali watu ni kiungo kikuu kati ya Mwajiri,
mwajiriwa na Mfuko hivyo kuona umuhimu wa kuwaelimisha wao ili waweze kutoa
ushauri kwa vijana ambao hawajajiunga na mfuko wowote.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment