Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro
akikata utepe kuashiria kuzinduliwa rasmi kwa Benki ya Access tawi la Mbeya.
|
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro
akiwa na viongozi wa Benki ya Access meza kuu katika hafla ya kuzindua tawi la
benki hiyo mkoani Mbeya.
|
. Meneja wa Mkoa wa Benki ya Access
Mbeya, Emmanuel Venance akitoa utambulisho kwa wageni mbali mbali waliohudhuria
sherehe za uzinduzi wa tawi la benki hiyo mkoani Mbeya.
|
. Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas
Kandoro akizungumza na wateja pamoja na wafanyakazi wa Benki ya Access
alipokuwa mgeni rasmi katika sherehe za uzinduzi wa tawi la benki hiyo jijini
Mbeya.
|
Mwakilishi wa Benki ya Access kutoka
Makao makuu jijini Dar es salaam, Sebastian Gaissert, akitoa hotuba yake katika
sherehe za uzinduzi wa tawi la benki hiyo mkoani Mbeya.
|
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dk. Norman
Sigallah King akijadiliana jambo na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro.
|
Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya wakifungua akaunti katika Benki ya Access baada ya kuzinduliwa rasmi. |
Viongozi wa Benki ya Access wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya. |
|
Wafanyakazi wa Benki ya Access tawi la Mbeya wakishangilia jambo katika sherehe za uzinduzi wa tawi hilo. |
wakitoa burudani wakati wa sherehe za uzinduzi wa benki hiyo tawi la Mbeya |
Watumishi na wafanyakazi wote wa benki ya Access tawi la Mbeya wakiwa kwenye picha ya pamoja. |
Muonekano waJengo la Benki ya Access tawi la Mbeya |
MKUU
wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro,amewataka wakazi wa mkoani hapa kuacha kasumba
ya kuhifadhi fedha nje ya mfumo wa kibenki kwa kuwa unadidimiza ukuaji wa kiuchumi.
Kandoro
aliyasema hayo alipokuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa tawi la Benki ya
Access katika hafla iliyofanyika kwenye viunga vya tawi hilo Mafiati jijini
Mbeya.
Alisema
katika utafiti uliofanyika mwaka 2013 ulibaini kuwa ni asilimia 7 tu ya wakazi
wa Mkoa wa Mbeya ambao hutumia mifumo ya kibenki kuhifadhi fedha zao huku
asilimia 93 wakihifadhi majumbani mwao.
Alisema
tabia ya kuhifadhi fedha majumbani haisadii katika kuongeza mzunguko wa fedha
bali huchangia kudidimiza uchumi wa Mkoa kutokana na fedha hizo kutoingia
kwenye mzunguko wa soko.
Aliongeza
kuwa kitendo cha kuhifadhi fedha majumbani pia huchangia kuwavutia majambazi
ambao huweza kuvamia na kuiba hivyo njia pekee ya kuhifadhi fedha ni kwa njia
ya benki.
Aidha
Mkuu wa Mkoa alitoa wito kwa watumishi wa benki kufanya kazi kwa uadilifu na
kuwa waaminifu kwa wateja wao kwa kuepuka kuiba fedha kwenye akaunti zao pamoja
na kuvujisha siri za ndani za akaunti ya Mteja.
“
Ni toe wito kwa watumishi epukeni kuvujisha siri za akaunti za wateja wenu,
wizi kwa njia za mtandao hivyo jengeni imani kwa wananchi kwa kufanya kazi kwa
uadilifu” alisema Kandoro.
Kwa
upande wake Mwakilishi wa Benki hiyo kutoka Makao makuu Dar es salaam,
Sebastian Gaissert, Benki hiyo imevutiwa kufungua tawi mkoani Mbeya kutokana na
kuwa miongoni mwa Mikoa yenye shughuli nyingi za kiuchumi na inayokua kwa kasi
kimaendeleo.
Alisema
sababu nyingine ya kufungua tawi Mkoa wa Mbeya ni kutokana na kuiunganisha
Tanzania na nchi jirani hivyo kuchochea shughuli za kibiashara pamoja na kuwa
tegemeo kwa kilimo cha mazao ya chakula na biashara.
Aliongeza
kuwa sababu ya pekee ni kuimarika kwa ulinzi na usalama hivyo kuipelekea benki
hiyo kuvutiwa na hali hiyo na kuona ni sehemu salama kwa ajili ya uwekezaji
mkubwa.
Alisema
tangu kufunguliwa kwa Tawi hilo Mkoani Mbeya Januari Mwaka huu zaidi ya mikopo
600 yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 1.5 imetolewa kwa wateja wao
pamoja na kufanikiwa kufungua akaunti mpya zaidi ya 1500.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment