Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Probesheni na huduma kwa jamii, Charles Nsanze, akimkaribisha mgeni rasmi |
Waandishi wa habari wakiwa makini kumsikiliza mgeni rasmi katika ufunguzi wa mafunzo juu ya adhabu mbadala kwa wafungwa |
Baadhi ya wawezeshaji katika mafunzo hayo |
Baadhi ya wawezeshaji katika mafunzo hayo |
Mr. Kawawa Mgungu (Senior Probation Officer) akiwasilisha mada katika mafunzo kwa Wanahabari. |
Washiriki wa Mafunzo wakiwa ukumbini kuendelea na mafunzo hayo. |
Picha ya pamoja |
WAANDISHI wa habari mkoani Mbeya wametakiwa kuisaidia Serikali katika kuihamasisha jamii kuhusu uwepo na utekelezaji wa adhabu mbadala kwa wafungwa.
Aidha imeelezwa kuwa jamii pia imetakiwa kuupokea na kuutekeleza mpango wa adhabu
mbadala kwa wafungwa kutokana na mpango huo kuiondolea serikali gharama kubwa
ya kuwahudumia waharifu badala yake mharifu ndiye anayeihudumia jamii.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Profesa Norman
Sigallah, alipokuwa akifungua mafunzo ya Utekelezaji wa adhabu mbadala kwa
wafungwa kwa Waandishi wa habari wa Mkoa wa Mbeya yaliyotolewa na Wizara ya
Mambo ya ndani katika Hoteli ya Gr Soweto jijini Mbeya.
Profesa Sigalla alisema adhabu
mbadala kwa wafungwa kutaisaidia jamii na serikali kupunguza gharama ambazo
zinatolewa kuwahudumia wafungwa pamoja na Askari wanaowahudumia kwa kulipia
chakula na mishahara hivyo kupitia adhabu mbadala mharifu huifanyia kazi jamii
katika kutekeleza adhabu yake.
Aliongeza kuwa Adhabu mbadala
ni suala geni katika jamii hivyo kupitia mafunzo kwa Waandishi wa habari
yatasaidia jamii nzima kuelewa na kuipokea ikiwa ni pamoja na kutekeleza zoezi
hilo pindi litakapoanza kutekelezwa kwa kupunguza wafungwa magerezani.
Alisema pia adhabu mbadala
ikianza kutekelezwa itaisaidia jamii kwa kuwa itakuwa ikimuona mharifu akiwa
anafanya adhabu yake pamoja na mharifu kujutia adhabu yake kutokana na kuifanya
hadharani ambapo kila mwananchi anaweza kupita na kumuana hivyo kila mwanajamii
kushiriki katika usimamizi.
Awali akimkaribisha Mgeni
rasmi, Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Probesheni na huduma kwa jamii, Charles
Nsanze, alisema Wizara ilipata msaada wa fedha kutoka shirika la Penal reform
international la nchini Uingereza kwa ajili ya mafunzo ya utekelezaji wa adhabu
mbadala kwa nchi za Afrika Mashariki.
Alisema Wizara ilichagua Mkoa
wa Mbeya kutekeleza mradi huo kutokana na kukua kwa Jiji la Mbeya na ongezeko
la uhalifu ambao unaweza kupelekea kuwa na msongamano wa wafungwa magerezani
hivyo njia ya kunusuru hali hiyo ni kutoa mafunzo kwa wanahabari ili kuijulisha
jamii kuhusu adhabu mbadala.
Nsanze aliongeza kuwa lengo la
kutoa mafunzo hayo kwa wanahabari ni kuutarifu umma mzima juu ya uwepo wa
adhabu mbadala itakayosaidia kupunguza wafungwa wasio na ulazima wa kutumia
vifungo wakiwa magereza, kuongeza idadi kubwa ya wafungwa walio nje ya vifungo
pamoja na kutii sheria za mahakama.
Alisema mbali na mafunzo hayo
kutolewa kwa wanahabari pia yatatolewa kwa Mahakimu wote Mkoa wa Mbeya,
wasimamizi wa wafungwa magerezani na wadau mbali mbali wakiwemo waendesha
mashtaka, mawakili, Polisi na askari magereza ambao watapewa mafunzo hayo
katika awamu tofauti.
Aliongeza kuwa lengo la Idara
hiyo ni kuishirikisha jamii na wafungwa katika utekelezaji wa adhabu mbadala na
kuwarudisha wafungwa katika jamii wakiwa salama na kupunguza msongamano wa
wafungwa magerezani.
Alisema faida ya adhabu mbadala
kwa wafungwa itamsaidia kuendelea kutumikia adhabu huku akiendelea kuhudumia
familia yake kuliko angekaa gerezani, kuepuka kunyoshewa vidole na jamii
kutokana na kutokuwa kwenye mavazi maalumu na kutekeleza adhabu yake kwa
kujichanganya na jamii nyingine.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment