Baadhi ya waandishi wa habari
MAMLAKA ya kudhibiti chakulana Dawa
Kanda ya Nyanda za juu kusini(TFDA) Mbeya imesema itaadhimisha wiki ya chakula
Tanzania kutoa elimu kwa wananchi.
Aidha Mamlaka hiyo pia imewashauri
wananchi kuzingatia usafi kabla na baada ya kula ili kuepukana na
magonjwa ya milipuko kwa kunawa mikono kabla ya kula, kuandaa chakula na baada
ya kutoka chooni.
Ushauri huo umetolewa na Kaimu Meneja wa
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA)Kanda ya Nyanda za juu kusini, Rodney
Alananga, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ikiwa ni
pamoja na kutoa taarifa ya maadhimisho ya wiki ya chakula Tanzania.
Alananga alisema wiki hilo
linaadhimishwa kuanzia Oktoba 20 hadi 26, mwaka huu ambapo kitaifa inafanyikia
katika viwanja vya Mwembeyanga Temeke jijini Dar es salaam na kwamba kila Kanda
itaadhimisha kwa shughuli mbali mbali zenye lengo la kuhamasisha wananchi
kuzingatia usafi kwenye chakula.
Alisema kikanda katika wiki hilo
watatumia muda mwingi kutoa elimu na kuhamasisha wananchi kwenye jamii kuhusu
umuhimu na madhara ya kutokujali usafi kwenye chakula, kutoa maonesho mbali
mbali ya bidhaa na kugawa vipeperushi vitakavyokuwa vikielimisha wananchi.
Alisema pia watahakikisha wanaleta
chachu kwa jamii ili kuleta mabadiliko ya kujenga tabia ya usafi,kukataa
kutumia chakula ambacho sio salama, kuzingatia mfumo mzima wa chakula kuanzia
uzalishaji hadi kumfikia mlaji kwa kuzingatia kanuni bora za chakula salama.
Alisema chakula salama ni kile ambacho
hakina dalili za kuingiliwa na uchafu wa aina yoyote ambao binadamu akitumia
anaweza kupata madhara ya muda mrefu au madhara ya papo hapo kutokana na uwepo
wa vijidudu, uchafu wa kawaida au kemikali.
Alisema kauli mbiu ya Wiki la chakula ni
Chakula salama ni msingi wa afya bora na maendeleo na kufafanua kuwa kauli mbiu
hiyo imelenga umuhimu wa kulinda afya kuzalisha na kuleta maendeleo ili
kumkwamua kiuchumi mwananchi.
Aliongeza kuwa kama watu hawatazingatia
usafi wa chakula wanaweza kupata madhara mbali mbali kama vile magonjwa ya
milipuko kama kipindupindu, vifo, matumbo ya kuhara,kukosa soko la chakula
kitaifa na kimataifa kutokana na kufungiwa baada ya kuona kinaleta madhara kwa
watumiaji.
Alisema ili kuepuka hali hiyo ni vema
kila mtu akazingatia usafi wa chakula hususani waandaaji na wamiliki wa
mahoteli ili kuhakikisha nyumba zao zinakidhi vigezo vya afya, wahudumu
kuzingatia usafi kabla ya kumhudumia mteja kwa kunawa mikono kwa maji safi na
sabuni, kutovaa pete na bangili mikononi na kwenye vidole, kupima afya zao
kabla ya kuanza kazi na kupima kila baada ya miezi sita.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment