Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akikata utepe kupokea vifaa Tiba
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro kushoto akimkabidhi vifaa tiba Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Seif Mhina
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Seif Mhina akiishukuru BAYLOR kwa Msaada huo
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akihutubia wananchi waliohudhuria hafla hiyo
Kaimu Mkurugenzi wa Kliniki ya BEYLOR Mkoa wa Mbeya Dkt. Theopista Masenga akisoma Risala mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro na wageni waalikwa wakati wa Hafla fupi ya kukabidhi vifaa hivyo
Hivi ndivyo vifaa tiba ambavyo vimetolewa na BAYLOR
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akipata maelekezo ya Moja ya vitanda hivyo hinavyofanya kazi
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro alioneshwa kabati la kisasa linalotumika kuhifadhia dawa na Chakula.
Baadhi ya watumishi wa BAYLOR
Baadhi ya wananchi waliofika katika Hafla hiyo fupi
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Mbeya Dkt. Mpoki Nulisubisya akiongea na wananchi waliofika katika Makabidhiano ya msaada wa vifaa tiba katika kituo cha BAYLOR
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akimsalimia mmoja wa watoto ambaye ni Mgonjwa anayesoma Darasa la kwanza, alifurahishwa na jibu la Mtoto huyo alipo ulizwa akiwa mkubwa anataka kuwa nani na kujibu kuwa angependa kuwa Dactari.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akiwa katika kitengo cha upimaji
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akiwa katika Kitengo cha Kifua kikuu
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akioneshwa eneo la mafunzo ambapo licha ya wagonjwa hao kupata matibabu lakini wanapatiwa mafunzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ushonaji
Picha ya pamoja
Shirika lisilo la
Kiserikali la BAYLOR Mkoa wa Mbeya
nchini Tanzania na Shirika la UNICEF la Umoja wa Mataifa limekabidhi vitanda 10
vyenye thamani ya zaidi shilngi milioni 10 kwa wilaya 5 za Mkoa wa Mbeya kwa
ajili ya watoto wenye utapia mlo na wanaoishi na maambukizi ya VVU Mkoani hapa.
Akikabidhi msaada huo
kwa niaba ya mashirika hayo Kaimu Mkurugenzi wa Kliniki hiyo ya BAYLOR Mkoani
Mbeya Dr. Theopista Jacob Masenga ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa
Mbeya Abbas Kandoro na kwamba wilaya tano zitanufaika na msaada huo.
Wilaya zilizonufaika
na msaada huo ni pamoja na Wilaya ya Mbozi,Mbeya,Mbarali na Rungwe katika
mpango wa mwaka 2014/2015 na wilaya zilizosalia zitaingizwa katika mpango wa
mwaka 2015/2016 ili kusogeza huduma karibu na wananchi na kuondoa usumbufu
wanaoupata wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo ambao wengi wao ni watoto.
Vifaa
vilivyokabidhiwa ni pamoja na vitanda 10 vya kisasa , magodoro 10 na makabati 10 ya
kuhifadhiwa dawa ambapo Kaimu Mkurugenzi
amesema vitasaidia kurahisisha utendaji wa kila siku wa huduma za tiba.
Akipokea msaada huo Mkuu
wa Mkoa aliyapongeza mashirika hayo kwa moyo wa kujitolea kuokoa maisha ya
watoto na kwamba serikali inaunga mkono juhudi kubwa zinazofanywa na mashirika
hayo na itaendelea kushirikiana nayo ili kuendelea kupunguza vifo vya watoto na
udumavu wa ubongo ambao usipodhibitiwa ndani ya siku 1000 maisha ya mtoto
yanakuwa yameharibika.
Kwa upande wake
mganga mkuu wa Mkoa Seif Mhina ameyashukuru mashirika hayo ambayo yanatoa
msaada mkubwa mkoani Mbeya na kwamba kituo hicho kinasaidia kupunguza
msongamano katika Hospitali ya Mkoa ambapo hupokea zaidi ya wagonjwa 300 kwa
siku.
Na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment