Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akiweka Jiwe la Msingi kuashiria ujenzi wa njia za kupitishia wagonjwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akiwahutubia wananchi waliofika katika Hafla hiyo
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mh. Norman Sigalla akitoa neno la Shukurani
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Seif Mhina akitoa Taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya
Mwenyekiti wa Kamati ya Marafiki Olise Ole Seenga akisoma Taarifa fupi juu ya ujenzi huo wa barabara za kupitishia Wagonjwa katika Hospitali ya Mkoa
Mshehereshaji Mwakilili akiendelea kutoa Mwongozo
Kaimu Meneja wa Kanda nyanda za Juu Kusini NMB Joel Uswege ambao pia ni Marafiki wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya akitoa neno
Meneja masoko wa Masoko wa AJ Technology Mbeya Eliah Susuwe ambao pia ni Marafiki wa Hospitali ya Rufaa Mbeya akitoa neno wakati wa sherehe hizo
Mmoja kati ya wagonjwa waliofika kupata huduma katika Hospitali ya Mkoa akiongea na Mkuu wa Mkoa kueleza jinsi huduma Bora zinazotolewa na wauguzi wa Hospitali ya Mkoa.
Katikati ni Mganga Mfawidhi Hospitali ya Mkoa Mbeya Glory Mbwile
Hii ni moja ya njia hizo
Hii ni Sehemu ya Mita 104 ambazo bado hazijakamilika
Picha ya Pamoja
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro amewataka
wananchi kuunga mkono juhudi ya Kamati ya Marafiki wa Hospitali ya Mkoa
walioamua kujenga njia za kupitishia wagonjwa zenye urefu wa mita 411.
Wito ameutoa
katika Hospitali ya Mkoa alipokuwa akiweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi
ambao umefadhiliwa na Kamati ya marafiki waliojitolea kujenga njia hizo
kutokana na adha kubwa wanayopata wagonjwa wanaofika katika Hospitali hiyo
kupata huduma mbalimbali za matibabu.
Akisoma
risala kwa Mkuu wa Mkoa Mwenyekiti wa Kamati ya marafiki Olise Ole Seenga amesema kuwa mpaka hivi sasa
wamebakiwa na mita 146 ambazo
hazijaguswa kabisa kutokana na ukosefu wa pesa jumla ya shilingi milioni 150
ili kukamilisha ujenzi huo.
Aidha Seenga
amesema kuwa mita 104 zimesakafiwa kwa saruji lakini hazijaezekwa kabisa hivyo
kuwaomba wananchi wajitokeze ili kukamilisha ujenzi huo ulioanza mapema mwezi
Mei mwaka huu baada ya kufanyika Harambee ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa
Mkoa ambapo jumla ya shilingi milioni 80 zilipatikana.
Kwa upande
wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro aliipongeza kamati ya
marafiki,Waandishi wa habari na wadau waliochangia fedha na mali kwa moyo wa uzalendo waliouonesha hata
kufanikisha kuanza kwa ujenzi huo.
Hata hivyo
Mkuu wa Mkoa alipokewa kwa furaha na wagonjwa waliokuja kupata huduma katika
hospitali ya Mkoa kutokana na utaratibu mzuri walioupanga ambao hautoi
upendeleo kwa wagonjwa na kuipongeza hospitali kwa utaratibu wa elimu kwa
wagonjwa kabla ya matibabu.
Kandoro
alihitimisha ziara yake kwa kuutaka uongozi wa Hospitali kuboresha mandhali ya
hospitali ili iwe faraja kwa wagonjwa wanaokuja kupata huduma na ametoa woto
kwa watu walioahidi kuchangia ujenzi huo kwa kushindwa kufanya hivyo
wanajidhalilisha utu wao na pia wanakwamisha juhudi kwa kuwa tamko lao
liliingizwa kwenye makisio.
Na Mbeya yetu Blog
1 comment:
Wanasiasa bwana. Waliochapa kazi wamewaweka kando. Wenyewe hao kimbelembele na mapicha. Mbona hata mganga mfawidhi, katibu afya mkoa hawaonekani kabisa. Tanzania bwana.
Post a Comment