Picha ya pamoja
BARAZA la Ushauri la watumiaji wa huduma
za usafiri wa Nchi kavu na Majini (Sumatra ccc) limetakiwa kubuni njia mbadala
itakayosaidia kuondoa changamoto ya usafiri kwa wanafunzi pindi wanapoenda na kutoka
mashuleni.
Mwito huo umetolewa na Kaimu Mkuu wa
Mkoa wa Mbeya, Dk. Michael Kadeghe, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbozi,
wakati akizindua Baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za usafiri wa nchi
kavu na majini Mkoa wa Mbeya, katika hafla iliyofanyika jana katika ukumbi wa
Haoteli ya Mtenda Sunset iliyopo Soweto Jijini hapa.
Kadeghe alisema hivi sasa kuna
changamoto ya usafiri kwa wanafunzi nchi nzima hali inayosababisha wanafunzi
kuhangaika kutafuta usafiri wa kuwarudishwa makwao kutokana na asilimia kubwa
kutoka mbali na shule ziliko hivyo kuwaletea usumbufu na kushundwa kuelewa
vizuri masomo yao.
Alisema kama baraza litaishauri vizuri
Serikali kuona inasaidia vipi katika kutatua changamoto hiyo ili kuwa na
usafiri maalumu kwa wanafunzi wa shule za kawaida ili kuwawezesha
kuondokana na usumbufu unaojitokeza na kusababisha Wanafunzi kurubuniwa na
baadhi ya madereva wanaowapa lifti.
Alisema hivi sasa wanafunzi wanarubuniwa
sana na baadhi ya madereva ambao siyo waaminifu ambapo huwapa msaada wa usafiri
kutokana na wanafunzi hao kusimamisha kila gari kutokana na magari mengi ya
abiria kuwakataa wanafunzi kwa madai kuwa wanapata hasara kwa kuwajaza
kwenye gari moja.
Aidha alitoa wito kwa baraza hilo
kushirikiana bega kwa began a Serikali pamoja na taasisi zingine ili kutatua
kero mbali mbali za wananchi kuhusiana na usafiri ambapo aliongeza kuwa magari
mengi ni chakavu na bado yanaendelea kutoa huduma pamoja na mwendo kasi
unaosababishwa na baadhi ya abiria kumchochea Dereva kuongeza mwendo.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa
Baraza hilo Taifa, Oscar Kikoyo alisema katika kuondoa baadhi ya wanafunzi
hususani wa kike kurubuniwa na madereva kutokana na kupewa misaada katika
magari yao Baraza limeanza kuunda Vilabu vya Mabaraza katika mashule
kwa lengo la kutoa elimu.
Aliongeza kuwa kazi ya Baraza siyo
kukamata magari yanayofanya kinyume na taratibu za usalama barabarani bali kazi
yao ni kushauri na kutoa elimu kwa wasafiri juu ya haki zao ili serikali
kupitia vyombo vyake iweze kuchukua hatua.
Alisema Mkoa wa Mbeya ni wa Saba
kuzindua Baraza hilo ambapo baada ya kuzinduliwa rasmi wataanza kazi kwa
kuwasilisha na kupokea maoni ya watumiaji wa usafiri, kupokea na kusambaza
maoni na taarifa juu ya haki za watumiaji wa sekta ya usafiri, kushauriana na
wadau kuhusu upatikanaji wa huduma bora na kuunda kamati za kushauriana nazo.
Baraza la Mkoa wa Mbeya lilizinduliwa na
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dk. Michael Kadeghe na kuwakabidhi vitambulisho
wajumbe Watano wanaounda baraza hilo ambao ni Saidi Madudu ambaye aliteuliwa
kuwa Mwenyekiti, Katibu Brandy Nelson na wajumbe wakiwa ni Jimmy
Ambilikile, Rosta Kihwani na Oswald Ngulangwa.
Naye katibu wa Baraza hilo Mkoa wa
Mbeya, Brandy Nelson ametoa wito kwa wadau wa usafiri Mkoa wa Mbeya kutoa ushirikiano
na baraza ili liweze kufikia malengo waliyowekewa kwa kuwasaidia kutoa taarifa
na maoni juu ya namna ya uboreshaji wa sekta ya Usafiri Mkoani Mbeya.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment